KUSHIRIKI TENDO LA NDOA KARIBU KABSA NA SIKU YA OVULATION
OVULATION
• • • • • •
Kushiriki tendo la ndoa karibu kabisa na siku ya ovulation, au siku yenyewe ya ovulation huongeza asilimia za kupata ujauzito. Ikiwa mwanamke atashiriki tendo la ndoa siku 6 na zaidi kabla ya siku ya ovulation, nafasi ya kupata ujauzito inakaribia 0%
Ikiwa atashiriki tendo la ndoa siku 4 kabla ya siku ya ovulation (ambayo itakuwa siku ya 5),nafasi ya kupata ujauzito ni walau 10%. Asilimia hizi huendelea kuongezeka kadri siku ya ovulation inavyokaribia ambayo hufikia hadi 30%.
DALILI ZAKE
Kuna dalili kuu 4 zinazotoa ishara ya kutolewa kwa yai (ovulation) ambazo ni Ute,Joto la mwili,maumivu pamoja na ishara zinaoonekana kwenye mlango wa kizazi.
Dalili zingine ni
• Kuongezeka sana kwa hamu ya kushiriki tendo la ndoa
• Maumivu ya nyonga
• Kuwasha na kuvimba kwa matiti
• Kuongezeka kwa uwezo wa kunusa na kutofautisha harufu mbalimbali za vitu
• Sehemu ya nje ya uke (mashavu) au uke wenyewe kuonekana umevimba kwa baadhi ya wanawake