Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI

HEDHI

• • • • • •

MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI 


 Ni hali ya mifuko ya mayai ya mwanamke (ovari) kutokomaza mayai na kuyaachilia ili yarutubishwe na mbegu za kiume


Hata kama unapata hedhi haimaanishi kwamba kila unapopata hedhi yai limeachiliwa, unaweza kupata hedhi na wakati yai halikupevuka na kuachiliwa na dalili kubwa ya tatizo hili ni pale mwanamke anapata hedhi vizuri ila hashiki ujauzito.


DALILI 

~ Mara nyingi wanawake wenye tatizo hili wanakua na mzunguko usioeleweka. Kama unapata mzunguko wenye siku chini ya 21 au zaidi ya 35 unaweza kuwa na tatizo hili. 


~ Na kama mzunguko wako una cku kati ya 21 hadi 34 lakini zinabadilika kila mwezi inaweza kua ni tatizo hili.

Mfano mwezi fulan umepata mzunguko wa siku 28 ulofata siku 30 ulofata siku 34.

.

TATIZO HILI NI MOJA YA UGUMBA

Tatizo hili ni mojawapo ya ugumba kwa wanawake. Ina maana usipovusha yai kunakua hakuna yai la kurutubishwa ili kutengeneza mtoto. Hvyo huwezi kupata ujauzito yai lisipopevuka. Mwanamke anapokua na Ovulation isiyoeleweka anakua na chance ndogo ya kushika ujauzito.


UTAJUAJE KAMA UNA TATIZO HILO??

Unaweza kufahamu kama una hilo tatizo ikiwa utakuwa na dalili zifuatazo :


1.Kukosa ute unaovutika kama ute wa yai


2.Utando unaotengenezwa kwenye mji wa mimba kua mwembamba sana


3.kiwango kidogo cha hormone ya progesterone


4.kuwa na kipindi kifupi cha lutea (luteal phase) hiki ni kipindi baada ya yai kuachiliwa ambapo kinapaswa kua si chini ya siku 14.


4.kutokua na mabadiliko ya Joto la mwili (basal body temperature)


VISABABISHI VYA TATIZO HILI 


1.Mvurugiko wa hormone ,hii ndo chanzo kikubwa.

2.uzito uliopita kiasi

3.kufanya mazoez sana kupitiliza

4.hormone ya maziwa (prolactin hormone ) kuwa juu

5.ukomo wa hedhi

7.Stress,mfadhaiko na msongo wa mawazo

.

Unaweza kugundua tatizo hili kwa kujipima mwenyewe nyumbani. Kwa kufata chart ya joto na ute unapoona hakuna mabadiliko ya joto baada ya cku ya 14 basi ina maana hujapevusha yai. Pia unapokosa ute unaovutika ina maana hujapevusha yai.

Kw ushauri zaidi,elimu au Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.