Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
afyatipsMagonjwamagonjwa ya wanaumemagonjwa ya wanawakemagonjwa ya watoto

UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA LASSA


UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA LASSA


Imeandaliwa na @doktamathew

Katika siku za hivi karibuni yapata miezi mitatu sasa kumekua taarifa sana zilizosambaa juu ya ugonjwa wa homa ya corona,mlipuko ambao ulitokea katika jiji la wuhan huko nchini China,na kirsi cha corona kinaaminika kimetoka kwa popo japokua haijafahamika ni njia zipi corona katoka kwa popo na kumuingia binadamu.

Mwanzoni mwa mwaka huu kumeripotiwa mlipuko mpya wa homa ya lassa huko nchini Nigeria,homa ambayo imewapata watu Zaidi ya 84 na kuua takribani watu 24,kati ya walokufa wamo madaktari wawili na mwanamke mjamzito mmoja;hii ni kulingana na NCDC


HOMA YA LASSA NI NINI?? Ni homa kali ya virusi isababishwayo na kirusi aitwaye Lassa mammarenavirus.Homa hii ipo nchi za afrika magharibi kama Benin, Ghana, Guinea, Liberia, Mali, Sierra Leone, Togo and Nigeria;vile vile zipo nchi nyingine ambazo zina homa hii ambazo bado hazijaripotiwa. Zipo pia taarifa ya kuwepo kwa homa hii katika nchi za Marekani,Uingereza na China na inaaminika homa hii imeingizwa huko kupitia watalii waliokuja kutalii katika nchi hizo..Homa iligundulika kwa mara ya kwanza mwaka 1969 katika Kijiji cha Lassa nchini Nigeria,ambapo manesi wawili waliokua wanapata homa ambayo hazieleweki eleweki. Homa ya lassa huwapata Zaidi ya watu 300,000 kila mwaka na husababisha vifo vya watu Zaidi ya 5000 kila mwaka.kumekua ongezeko la ghafla la mlipuko wa homa ya lassa katika kipindi cha mwaka 2017 na mwaka 2018 ambapo Zaidi ya watu 430 walithibitishwa kua na homa hii na asilimia 25 ya hao watu walipoteza Maisha;hali hii imezua maswali kwa watafiti juu ya uwezekano wa huyu kirusi kua amebadilika na huenda tukawa tunaongelea kirusi mpya


PICHA:Sciencedirect.com

.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass