Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Sukari ya Muda Mrefu na hatari ya Kupata tatizo la Moyo kushindwa kufanya Kazi(Heart failure)

Sukari ya Muda Mrefu na hatari ya Kupata tatizo la Moyo kushindwa kufanya Kazi(Heart failure)

Kadri Mtu anavyokuwa na Ugonjwa wa Sukari kwa muda mrefu ndivo hatari ya Kupata tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi(Heart failure) huongezeka zaidi,

Hii ni kwa Mujibu wa Utafiti uliofanywa kwa watu karibu 24,000 wenye Kisukari ndani ya UK Biobank

Majibu ya Utafiti huu yalionyesha, kuna Uhusiano wa karibu sana kati ya Muda wa kuwa na Ugonjwa wa Sukari(Diabetes duration) pamoja na tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi yaani Heart failure.

Pia utafiti ulionyesha;mbali na Tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi,Kadri Sukari inavyokuwa ya muda mrefu huweza kusababisha uwezo wa figo kufanya kazi kupungua na Kusababisha Matatizo ya FIGO pia,

The UK Biobank study:

Utafiti huu kwa Mara ya kwanza ulianza kufanyika nchini China na ulihusisha takwimu(data) Kutoka kwa Watu 23,754 wenye ugonjwa wa Kisukari aina zote mbili- type 1 au type 2 diabetes,

Na hawakuwa na tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi(heart failure) wakati utafiti unaanza.

Washiriki hawa,walifanyiwa follow-up kwa Muda wa miaka 11.7, na Ndipo katika kipindi hichi, Washiriki 2081 walipatwa na tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi-heart failure.

Na katika Utafiti huu,Washiriki waligawanywa kwenye Makundi Manne..

  1. Wenye Ugonjwa wa Kisukari kwa Muda wa chini ya Miaka 5(< 5 years)
  2. Wenye Ugonjwa wa Kisukari kwa muda wa Miaka 5-9,
  3. Wenye Ugonjwa wa Kisukari kwa muda wa Miaka 10-14
  4. Pamoja na Wenye Ugonjwa wa Kisukari kwa Muda wa kuanzia miaka 15 au zaidi ya Miaka 15(≥ 15 years)

MATOKEO YAKE:

Kiwango cha Tatizo la Moyo kushindwa kufanya kazi(heart failure incidence) kiliongezeka kwa asilimia 32% kwa Watu wenye Ugonjwa wa Kisukari kwa kipindi cha Miaka 15 au zaidi ya miaka 15( ≥ 15 years),

ikilinganishwa na watu wenye Ugonjwa wa Kisukari kwa Muda wa chini ya Miaka 5( < 5 years).

HITIMISHO(CONCULSION):

Matokeo haya “yanaonyesha Uhusiano wa karibu sana kati ya muda wa ugonjwa wa kisukari na tatizo la kushindwa kwa moyo katika utendaji kazi wake,”

Kadri Muda wa kuugua ugonjwa wa kisukari unavyokuwa mrefu zaidi,ndivo unaweza kusababisha mabadiliko ya utendaji wa Moyo.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.