Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA TINEA VESICOLOR (PITYRIASIS VERSICOLOR

UGONJWA WA TINEA VESICOLOR (PITYRIASIS VERSICOLOR

Huu ni ugonjwa wa fangasi ya ngozi ambao hupelekea mgonjwa kua na mabaka mabaka meupe,meusi na maeneo mekundu mekundu katika ngozi yake, ugonjwa huu hushambulia sana maeneo ya mgongo ,mabegani na mikono juu ya kiwiko(proximal upper extrimities). Ugonjwa huu upo sana na maarufu miongoni mwa watu wengi tu na wengine huiona hali hii kama kawaida 

Ugonjwa huu husababishwa na hamira mpenda mafuta aitwae Malasezzia furfur,Malasezzia globosa na Malasezzia sympodialis,hamira huyu hupenda sana kuwashambulia vijana na watu wenye umri wa kati.ugonjwa huu hauhusiani na uchafu ama usafi wa mtu


WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU

1) Kua kijana au mtu mwenye umri wa kati

2) Utapiamlo

3) Wenye kisukari,saratani na HIV


4) Walio kwenye maeneo ya joto

5) Walio kwenye maeneo yenye unyevu unyevu

6) Ujauzito

7) Watu wenye mvurujiko wa homoni

8) Watu wenye ngozi zenye mafuta


Najua una jiuliza unatibikaje? Labda nikuondoe wasi wasi ugonjwa unatibika na unaisha.

• • • • • •

DALILI ZA UGONJWA HUU


Kama nilivokwisha kusema hapo juu ugonjwa huu kwa asilimia kubwa humfanya mtu awe na ngozi kavu maeneo ya mgongoni na mikononi na ambayo anakua na mabaka mabaka meusi na meupe na wakati mwingine yamechanganyika na mabaka mabaka mekundu. Wagonjwa walio wengi hua hawapati muswaso kama ilivo kwa magonjwa mengine


MATIBABU YA UGONJWA HUU

Kwa bahati nzuri ugonjwa huu unatibika vizuri tu na unaisha;japo mabaka mabaka yalokwisha kutokea yanaweza kuchukua miezi kadhaa kuisha na kurudi hali yako ya zamani. Zipo dawa za kupaka na kuogea ambazo zinafanya kazi vizuri sana. Kama za kupaka zikishindwa kufanya kazi basi itabidi utumie dawa za vidonge na tatizo litakua limekwisha. Kwa hiyo ndugu zanguni kama unaona una dalili za ugonjwa huu basi usisiste kufika hospitali ili uchekiwe na kupewa dawa sahihi.

Mwisho.

NA Dr.Ngimi

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.