Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
afyatipsMagonjwamagonjwa ya wanaumemagonjwa ya wanawakemagonjwa ya watoto

VIHATARISHI 16 VYA KUPATA FANGASI UKENI

FANGASI UKENI

• • • • • •

Vihatarishi vya Fangasi wa ukeni ni;


1. Kutumia sana dawa aina ya detergents kwenye sehemu za siri au douches (vifaa vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia maji yaliyochanganywa na siki au antiseptic yoyote ile) kwa sababu hali husababisha kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina ya lactobacilli


2. Kutumia sana madawa aina ya antibiotics, steroids ambayo yana tabia ya kushusha kinga ya mwili


3. Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini ambayo husababisha mabadiliko katika sehemu za siri na hivyo kufanya kuwepo kwa ukuaji wa kasi wa fangasi hawa


4. Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa kinga ya mwili). Hata hivyo ieleweke hapa kuwa si kila mjamzito hupatwa na maambukizi haya.


5. Matumizi ya dawa za kupanga uzazi (vidonge vya majira)


6. Upungufu wa kinga mwilini kutokana na magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina yoyote ile, ugonjwa aina ya mononucleosis na nk. 


7. Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS)


8. Matibabu ya homoni (hormonal replacement therapy) kutokana na sababu mbalimbali


9. Matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa wale wenye matatizo ya uzazi (infertility treatment)


10. Msongo wa mawazo (stress)


11. Utapia mlo (malnutrition)


12. Kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto sana sehemu za siri kwa muda mrefu kama nguo za kuogelea (swimwear), nguo za ndani (chupi)  zilizotengenezwa kwa kitambaa aina ya nylon, nguo za ndani zinazobana sana nk.


13. Kujamiana kwa njia ya kawaida mara tu baada ya kujamiana  kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi venye glycerin wakati wa kujamiana pia yamehusishwa na maambukizi haya.


14. Kuvimba kwa tezi la koo (goiter)


15. Saratani ya tezi la koo (thyroid cancer)


16. Wanawake wenye umri wa miaka kati ya ishirini na thelathini wapo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi haya wakati wale ambao wameshaacha kupata hedhi au wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa hawako kwenye hatari kubwa. 


#afyabongo #drtareeq


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass