Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

VYAKULA MUHIMU KUKUWEZESHA KUPATA UJAUZITO

UJAUZITO

• • • • • •

VYAKULA MUHIMU KUKUWEZESHA KUPATA UJAUZITO.


Mwanamke aliye katika umri wa kuzaa anahitaji apate lishe bora ili kumwezesha kupata ujauzito pale anapohitaji. 


Vyakula muhimu kwa uzazi

Vipo vyakula vingi sana lakini kwa leo tutaona baadhi na vingine tutaona siku nyingine.


1.AMINO ACIDS; Jamii hii ya chakula ni muhimu kwa uzalishaji wa mayai na hata mbegu za kiume. Hupatikana kwenye vyakula vya protini mfano nyama, maharage, kunde, choroko, njegere, soya na jamii zote za kunde na nyama aina zote pamoja na mayai.


2.VITAMINI A: Ni muhimu pia katika uzalishaji wa vichocheo vya uzazi  na kusaidia uzalishaji wa mayai na ute wa uzazi na kuboresha hamu ya tendo la ndoa.


Vitamini A hupatikana katika mayai, maembe, ndizi mbivu, mboga za majani kama mchicha, matembele, mnavu, kisamvu na majani ya maboga na jamii zake. Hupatikana pia katika maziwa na mafuta ya samaki.

Vitamini A pia ni muhimu hata wakati wa ujauzito na kwa watoto wadogo.


3.Vitamin B na Folic Acid,

Vitamini B zipo aina nyingi takriban sita, hatutaweza kuchambua moja baada ya nyingine leo ila tutakuja kuona kwa undani baadaye na ni muhimu sana katika uzalishaji wa mayai ya uzazi na kuepusha kasoro kwa mtoto atakayezaliwa.

Vitamin B haiwezi kufanya kazi endapo mhusika atakuwa anavuta  sigara au anabwia ugoro, anakunywa pombe ya aina yoyote pia kama muda wote hayupo sawa kisaikolojia.


4.Vitamini C, Vitamini E na madini ya chuma pia vina umuhimu mkubwa katika uzazi, madini kama Magnesium husaidia ubora wa uzazi na kuzuia mimba kuharibika mara kwa mara.

Jamii ya vyakula hupatikana katika mayai ya kuku, mafuta ya kupikia yatokanayo na mbegu mfano alizeti, mawese na mengineyo, karanga, maparachichi, viazi vitamu na mboga za majani.


5.Madini ya chuma hupatikana katika nyama mfano maini, figo, moyo, mayai, samaki na dagaa, mbegu za mafuta mfano alizeti.


6.Madini ya magnesium ni muhimu na hupatikana katika mboga za majani, mtama, mchele ndizi. Magnesium huzuia mimba kuharibika mara kwa mara na kukaa vizuri baada ya kurutubishwa.

.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.