Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE NINI KINASABABISHA UWE NA UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA?

PRESHA

• • • • • •

JE NINI KINASABABISHA UWE NA UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA?



Kiwango cha kawaida cha Presha ni kati ya 90-140 mmhg ya juu na chini ni 60-90mmhg, Mfano; Kama una presha,90/60mmhg mpaka 140/90mmhg,upo kwenye kiwango sahihi cha Presha kikizidi hapo au kupungua tayari una tatizo la Presha(ya kupanda au kushuka).


Kama inavyofahamika kwamba kuna aina mbili za Presha au shinikizo la Damu. Kuna Presha ya kupanda na kuna presha ya kushuka, Na kila aina kuna sababu zake zinazichangia kutokea. Ila kwa leo tunazungumzia kuhusu presha ya kupanda,zipi ni sababu za Presha hii?



VITU VINAVYOCHANGIA UWE NA UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA


1. Kuwa na Msongo wa mawazo ambayo hayaishi kila siku


2. Vitu vyote ambavyo vinaweza kukupa hofu na wasiwasi kila mara Mfano; misiba,ajali,magonjwa N.k


3. Kuwa na Umri mkubwa,Tafiti zinaonyesha kwamba watu ambao wana umri wa zaidi ya miaka 70 hupatwa na tatizo la Presha ya kupanda zaidi ya wale walio na umri mdogo.


4. Watu ambao wana uzito mkubwa au wanene wapo katika hatari ya kupata ugonjwa wa Presha ya kupanda


5. Tatizo la presha ya kupanda katika familia yenu, huweza kuchangia na wewe kupatwa na shida hiyo


6. Matumizi ya chumvi nyingi wakati wa kula chakula


7. Unywaji wa Pombe kupindukia huweza kuwa chanzo kikubwa cha tatizo la Presha ya kupanda


8. Kukosa Usingizi au kukosa mda wa kutosha wa kulala


9. Kuwa na magonjwa mengine kama kisukari,Vidonda vya tumbo N.K


MADHARA YA PRESHA YA KUPANDA


– Huweza kukusababishia Kifo


– Huweza kusababisha tatizo la mshipa wa kichwani kupasuka na kuvuja damu


– Huweza kukuletea hali ya kizunguzungu na kukudondosha chini


– Huweza kukusababishia magonjwa ya Moyo


– Huweza kusababisha upofu wa macho


– Huweza kusababisha matatizo ya Figo


– N.K


MAMBO YA KUZINGATIA KAMA UNA UGONJWA WA PRESHA YA KUPANDA


• Jenga tabia ya Kufanya mazoezi mara kwa mara


• Punguza uzito au unene kama una shida hyo


• Acha kula chumvi nyingi kwenye chakula hasa hasa ile chumvi ya kuongezea baada ya chakula kuiva


• Epuka matumizi ya pombe


• Pata mda wa kutosha wa kulala baada ya kazi za kila siku



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.