Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

ENDAPO MDUDU ATAINGIA KATIKA SIKIO LAKO

AFYA YA SIKIO

• • • • • •

ENDAPO MDUDU ATAINGIA KATIKA SIKIO LAKO


NINI CHA KUFANYA?


1. Elekeza kichwa chako kuelekea juani. Kama ni gizani/usiku elekeza kwenye chanzo cha mwanga kama taa/tochi. Mdudu huweza kufuata mwanga na kutoka sikioni


2. Chukua kipande kidogo cha tufaha(apple) kiweke jirani na sikio lako. Mdudu huvutiwa na harufu yake na huweza kutoka nje


3. Mdudu aingiapo sikioni huweza kunasa katika nta(earwax) au huweza kudhoofika/kuishiwa nguvu ya kutoka nje hivyo, Inamisha kichwa upande kwa chini na mtu mwingine akutie mafuta ya zaituni(olive oil) ama mafuta mengine yatokanayo na mimea (vegetable oil) au baby oil kwenye sikio lenye mdudu. Mafuta yenye uvuguvugu(sio ya moto) hufaa zaidi. Mafuta yakisha ingia ruhusu yakae kwa muda wa dakika moja hivi halafu ruhusu yatoke kwa kuinamisha sikio yanapotoka hutoka na mdudu. Unapoinamisha sikio livute nyuma kwa juu ili kuruhusu njia (ear canal) kwa mdudu kutoka.


4. Kama hakuna ahueni, Weka maji ya uvuguvugu(sio ya moto) sikioni ukiwa umeinama na kulivuta sikio nyuma juu. Mdudu huweza kutolewa pamoja na maji hayo


MUHIMU: Kama haya yote hayajafanikisha kumtoa mdudu, Fika Hospitali!


ENDAPO MDUDU ASIPOTOKA MADHARA YANAYOWEZA KUTOKEA


1. Maumivu makali ya sikio


2. Kupoteza usikivu


3. Kuvuja damu sikioni


4. Maambukizi (infection)


5. Kutoboka kwa ngoma ya sikio (eardrum)


Cc: @_afyazone



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.