Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MADHARA YA KUPAKA MATE KWENYE SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE WAKATI WA TENDO LA NDOA.

MATE

• • • • • •

MADHARA YA KUPAKA MATE KWENYE SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE WAKATI WA TENDO LA NDOA.

Watu wengi  hawafahamu kwamba kuna madhara ya kupaka mate kwenye sehemu za siri za Mwanamke wakati wa tendo la Ndoa. Mate hukaa mdomoni na yana kazi zake kwenye Mdomo, Lakini endapo yatatumiwa kinyume na matumizi yake huweza kuwa chanzo kikubwa cha kusambaza magonjwa.

MATE NI NINI? NA YANA KITU GANI NDANI?

Tuchambue kidogo kuhusu mate,vitu vinavyounda mate pamoja na kazi za mate kabla ya kuangalia madhara ya kupaka au kuweka mate kwenye sehemu za siri za mwanamke.

Mate ni mchanganyiko wa vitu vitatu(3) ambavyo vipo mdomoni na vitu hivo ni;

(i) Ute ute

(ii) Maji maji

(iii) Pamoja na enzyme au kimeng’enya kinachojulikana kwa Jina la Ptyalin au Salivary Amylase.

Na vitu hivi vitatu kila kimoja kina kazi yake tofauti na kingine,ambapo kwa ujumla wake hukamilisha utendaji kazi mzuri wa mate kwa kazi iliyokusudiwa.

• Ptylin au Salivary amylase, hii huhusika na kufanya kazi ya kumeng’enya chakula na kukibadilisha kutoka Hatua moja kwenda nyingine Mfano;kubadilisha Wanga au kwa kitaalam Carbohydrate kuwa Sukari iliyopo kwenye fom nyepesi au kwa kitaalam tunaita Maltose

• Maji maji hufanya kazi ya kusaidia kukiyeyusha chakula kilichopo mdomoni

• Ute ute hufanya kazi ya kukifanya chakula kuwa katika hali ya utelezi na urahisi wa kumezeka.

Hivo basi Kwa ujumla wake naweza kusema kwamba, Maji yatalainisha chakula chako mdomoni,Enzyme(Salivary amylase) atafanya kazi ya kukivunja vunja, wakati huo Ute utakifanya chakula chako kiteleze na kupita kwa urahisi kutoka mdomoni, kupitia Njia ya chakula, na kwenda tumboni.

MADHARA YA KUPAKA MATE KWENYE SEHEMU ZA SIRI ZA MWANAMKE WAKATI WA TENDO LA NDOA.

Mbali na kazi za mate pamoja na vitu vinavyounda mate nilivyovitaja hapo juu, Mate pia huweza kuchanganyika na vimelea vya magojwa mbali mbali kama vile; Bacteria pamoja na Fangasi, Hapa ndipo tatizo huanza.

Sasa endapo utatoa mate kutoka mdomoni na kupeleka kwenye sehemu za siri za Mwanamke,tafsri yake unafanya kazi nyingine ya kuhamisha Bacteria,Fangasi pamoja na vimelea vingine vya Magonjwa, kutoka mdomoni kwenda ukeni na kupelekea maambukizi mengine kwenye via vya uzazi vya mwanamke ambayo hakuwa nayo.

️KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

2 Comments

  1. Pia doctor ongezea kuwa mate ya kitu kiitwacho cofactor Mg ambayo ni maalumu kwa kusaidia enzyme ya salivary amylase ifanye KAZI yake sawasawa

    Pia doctor mate ni mojawapo ya medium itumiwayo na kundi la virusi waitwao human papilomae virus kuishi kwasababu Yana optimal pH inaowasaidia kuishi hvy basi kama mate yatatumika wakati wa tendo basi Kuna uhakika wa virus hivi kuingia kwenye uzazi wa mwanamke nakuleta madhara

    Kumalizia , mate yakiwekwa kwenye Ute yaan asilimia 85 yaku ua mbegu za kiume

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.