Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU UGONJWA WA FANGASI(karibu darasa afya)

 FANGASI

• • • • •

MASWALI NA MAJIBU KUHUSU UGONJWA WA FANGASI(karibu darasa afya)


SWALI 1: Je kuna aina ngapi za ugonjwa wa Fangasi?


MAJIBU; Tatizo la fangasi limetajwa na kugawanywa kutokana na maeneo mbali mbali ambayo fangasi hushambulia katika mwili wa binadamu Mfano;


1. kuna fangasi wa sehemu za siri


2. Kuna fangasi wa kwenye damu


3. Kuna fangasi wa kooni


4. Kuna fangasi wa miguuni


5. Kuna fangasi wa kichwani


6. Kuna fangasi wa kwenye mikono


7. Kuna fangasi wa mdomoni


8. Kuna fangasi wa kwenye ulimi


9. Kuna fangasi wa kwenye ngozi 


N.K


SWALI 2: je zipi ni dalili za ugonjwa wa fangasi sehemu za siri kwa mwanaume na mwanamke?


MAJIBU; Dalili za ugonjwa wa fangasi kwa mwanaume na mwanamke ni pamoja na;


– Kuwashwa au kupata muwasho sana sehemu za siri ikiwa ni pamoja na ukeni,kwenye ngozi ya korodani za mwanaume N.K


– Ngozi ya korodani kwa mwanaume na mashavu ya uke kwa mwanamke pamoja na eneo linalotenganisha kati ya njia ya haja kubwa na sehemu za siri kubadilika rangi na kuwa nyekundu


– Kupatwa na vidonda pamoja na michubuko maeneo ya sehemu za siri


– Kutokwa na uchafu sehemu za siri, wenye harufu, rangi na mzito kama maziwa mgando kwa mwanamke


– Wakati mwingine kupatwa na maumivu sana na hali ya kuungua sehemu za siri kwa mwanamke wakati wa kufanya mapenzi


SWALI 3: Je ugonjwa wa fangasi sehemu za siri una madhara yoyote?


MAJIBU; Tatizo la fangasi sehemu za siri lina madhara mengi hasa pale likiwa sugu,miongoni mwa mazara hayo ni pamoja na;


– kuwashwa sehemu za siri hali ambayo huwa kero hata ukiwa mbele za watu


– Kutokwa na uchafu wenye harufu kwa mwanamke


– Maumivu wakati wa tendo la ndoa


– Kupata shida ya kubeba mimba au kushika ujauzito


N.K



SWALI 4: je fangasi sehemu za siri ina tiba?


MAJIBU; Ugonjwa wa fangasi sehemu za siri huhusisha matibabu mbali mbali kama vile; matumizi ya dawa aina ya Clotrimazole ambapo kuna Cream ya kupaka sehemu za siri pamoja na tube za kudumbukiza ukeni, Kuna Fluconazole N.K



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.