Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MATUMIZI YA DAWA AINA YA SILDENAFIL CITRATE (VIAGRA)(kutibu uume kushindwa kusimama)

DAWA

• • • • • •

MATUMIZI YA DAWA AINA YA SILDENAFIL CITRATE (VIAGRA)(kutibu uume kushindwa kusimama)

ni dawa inayotumika kutibu tatizo la kusimama kwa uume (erectile dysfunction) na shinikizo la damu kwenye mishipa.

Au wengine husema hutibu tatizo la nguvu za Kiume.

  Erectile dsyfunction ni tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri wakati wa kujamiiana au kushindwa kusimama kwa muda mrefu wakati wa tendo.

Tatizo hili husababishwa na vitu mbalimbali vikiwemo ajali,madawa,msongo wa mawazo n.k

ANGALIZO/TAHADHARI: Ni hatari sana kutumia dawa hizi pasipo vipimo pamoja na maelekezo maulumu au ya kina kutoka kwa Wataalam wa afya,

Dawa hizi hutumika kwa kundi maalumu sio kila mtu anachukua tu nakutumia. ni hatari sana kwa afya yako na hata huweza kusababisha KIFO, kama ambavyo kuna matukio mengi ya Wanaume kufariki baada ya kutumia dawa hizi.

 VIAGRA ZINAFANYAJE KAZI?…

 Viagra huongeza msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume na kuufanya usimame na uwe mgumu wa kujamiiana.Kwa kawaida viagra huanza kufanya kazi dakika 30-60 baada ya kumezwa na hutumika wakati mtu anataka kujamiiana.

  Baada ya tendo kumalizika uume unatakiwa utulie(loose erection) baada ya masaa manne.

HUPASWI KUTUMIA VIAGRA KAMA:-

 i.Umetumia dawa zenye nitrates kama nitroglycerine

ii.Umetumia dawa zinazoitwa “poppers” kama amyl nitrate au amyl nitrite na butyl nitrate

iii.Una mzio (allergy) na viambatanisho (ingredients) zilizotumika kutengeneza viagra.

MADHARA YA KUTUMIA VIAGRA NI PAMOJA NA:

i.Uume kusimama mda mrefu kupitiliza (priapism)

ii.Kupoteza uwezo wa kuona kwenye jicho moja au yote kwa ghafla

iii.Kupoteza uwezo wa kusikia ghafla

iv.Kupatwa na kizunguzungu

v.Maumivu ya kuchwa

vi.Maumivu ya misuli

vii.Mshtuko wa moyo (heart attack)

viii.Kiharusi (stroke)

ix.Kifo/VIFO, kuna matukio mengi ya wanaume kufa baada ya kutumia dawa hizi hovio pasipo maelekezo maalumu au yakina kutoka kwa wataalam wa afya

NB: EPUKA MATUMIZI YA DAWA HIZI HOVIO,NI HATARI SANA KWA AFYA YAKO.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.