Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANZO CHA TATIZO LA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA BAADA YA KULA CHAKULA

 KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA BAADA YA KULA CHAKULA


Tatizo hili huweza kumtokea mtu yeyote bila kujali jinsia wala umri, hapa nazungumzia uwepo wa tatizo hili la kichefuchefu na kutapika baada ya kula chakula kwa wanawake na wanaume, watoto,vijana na watu wazima.


Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa tatizo hili, na sababu hizi nimeziorodhesha katika makala hii hapa chini


CHANZO CHA TATIZO LA KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA BAADA YA KULA CHAKULA


– Hali ya kuwa mjamzito ambapo asilimia kubwa ya wakina mama wajawazito lazima wapatwe na tatizo hili la kichefuchefu pamoja na kutapika baada ya kula chakula


– Hali ya kichefuchefu na kutapika baada ya kula kwa mtu ambaye yupo safarini


– Matumizi ya baadhi ya dawa huweza kuleta hali hii


– Kuwa na matatizo kwenye kifuko cha nyongo ndani ya Ini


– Kula chakula ambacho kina sumu au viambata vya sumu


– Kuwa na hali ya hisia kali pamoja na msongo wa mawazo wakati wa kula


– Kula haraka haraka


– Kula chakula kingi kupita kiasi kwa mara moja


– Kuwa na maambukizi mbali mbali ya magonjwa kwenye mfumo mzima wa chakula ikiwa ni pamoja na tumbo,utumbo mdogo,n.k


– Kuwa na tatizo la vidonda vya tumbo


– Hali ya allergy kutokana na aina ya chakula flani ulichokula


– Kuwa na tatizo la appendix au kidole tumbo


– Kuwa na tatizo la kansa


– Kuwa na tatizo kwenye ubongo


– Kuziba kwa Njia ya chakula ikiwa ni pamoja na utumbo mdogo


– Kuwa na magonjwa mengine kama Malaria, Homa ya matumbo au typhoid n.k



MATIBABU YA TATIZO HILI


– Matibabu ya tatizo hili hutofautiana kwa kutegemea na chanzo chake, hivo kama una tatizo hili ni vizuri kwenda hospital kwa ajili ya vipimo na uchunguzi zaidi na ndipo hatua za kimatibabu zianzie hapo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.