Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA ALDOSTERONISM(chanzo,dalili,tiba)

 TATIZO LA VICHOCHEO MWILINI

• • • • •

TATIZO LA ALDOSTERONISM(chanzo,dalili,tiba)


Aldosteronism hili ni tatizo ambalo huhusisha tezi aina ya Adrenal Gland kuzalisha  kwa kiasi kikubwa sana kichocheo aina ya Aldosterone kuliko ilivyokawaida.


CHANZO CHA TATIZO LA ALDOSTERONISM


– Kurithi vinasaba vya tatizo hili ndani ya familia au koo flani


– Kufanya kazi kupita kiasi kwa tezi zote mbili za Adrenal Gland


– Kuwa na shida ya kansa kwenye tezi moja au mbili ya adrenal Gland


– N.K



DALILI ZA TATIZO LA ALDOSTERONISM NI PAMOJA NA;


– Mgonjwa kupata kiu sana ya maji


– Mgonjwa kupata hisia za kukojoa kila mara


– Mwili kuchoka kupita kiasi


– Kuwa na shida ya presha kuwa juu


– Kuwa na tatizo la Kukaza kwa misuli ya mwili


– Kupata maumivu makali ya kichwa mara kwa mara

N.K


MATIBABU YA TATIZO LA ALDOSTERONISM

✓ matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake,ila kwa ujumla zipo tiba mbali mbali kama vile;


 matumizi ya dawa zinazozuia uzalishwaji wa kiwango kikibwa cha hormone ya Aldosterone pamoja na Kufanyiwa upasuaji na kuondolewa kwa tezi hizi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.