Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MOLAR PREGNANCY(chanzo,dalili na tiba)

 UZAZI

• • • •

TATIZO LA MOLAR PREGNANCY(chanzo,dalili na tiba)


Molar pregnancy ni hali ya ukuaji wa seli(trophoblasts) usio wakawaida ndani ya mfuko wa uzazi na kumfanya mwanamke kuonekana mjamzito na kuwa na dalili zote za mimba wakati hana mimba.


CHANZO CHA TATIZO LA MOLAR PREGNANCY


Tatizo hili la molar pregnancy hutokana na hitilafu katika urutubishaji wa yai ambapo hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo imeonekana kusababisha shida hii, japo kuna baadhi ya sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata shida hii kama vile;


– Mwanamke kujaribu kubeba mimba akiwa na umri mkubwa mfano zaidi ya miaka 35


– Mwanamke kujaribu kubeba mimba kwenye umri mdogo sana mfani chini ya miaka 18


– Kuwa na shida hii kwa hapo kabla


– Matumizi ya baadhi ya dawa hasa ambazo huhusu kuongeza au kupunguza vichocheo mwilini



DALILI ZA TATIZO LA MOLAR PREGNANCY

– Kwa mwanzoni mwanamke huanza kupata dalili zote za mimba lakini baadae huaza kuonyesha utofauti kama vile;

• Mwanamke kuanza kuvuja damu ukeni


• Mwanamke kupata maumivu makali ya nyonga na tumbo


• Mwanamke kutoa uchafu sana sehemu za siri


• Mwanamke kupata kichefuchefu sana na kutapika


• Tumbo kuongezeka kwa haraka sana kuliko kawaida na kuliko umri wa mimba


MATIBABU YA TATIZO LA MOLAR PREGNANCY

– Molar pregnancy haiwezi kuendelea na kukua kama mimba ya kawaida hivo mwanamke mwenye shida hii anatakiwa kwenda hospital kwa ajili ya vipimo zaidi na msaada wa kimatibabu


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.