Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANZO CHA CHUCHU KUUMA NA KUTOA DAMU

CHANZO CHA CHUCHU KUUMA NA KUTOA DAMU

Tatizo la matiti kukuuma,chuchu kuvimba,kuwa na vidonda,kutoa maji maji,kutoa usaha au damu, ni miongoni mwa matatizo ambayo hutokea kwenye titi,

Lakini katika makala hii tunazungumzia kuhusu chuchu kuuma sana pamoja na kutoa damu, Je hii ni dalili ya ugonjwa gani?

CHANZO CHA CHUCHU KUUMA NA KUTOA DAMU

– Moja ya sababu kuu ya chuchu kuuma sana pamoja na kutoa damu ni tatizo la Saratani ya matiti au kwa kitaalam hujulikana kama Breast cancer.

Mara nyingi mtu mwenye tatizo la Kansa ya Titi au matiti huanza kutoka damu kwenye chuchu ambayo huambatana na;

  •  Maumivu makali ya titi
  • Chuchu kuingia ndani zaidi
  •  titi moja ambalo limeathiriwa kubadilika umbo na kuwa kubwa kuliko lingine
  •  kuwa na vitu vigumu kwenye titi mithili ya punje ya harage au mchele ambavyo huweza kushikika mpaka maeneo ya kwapani
  •  Titi kuvimba
  • Ngozi ya titi kubadilika rangi na kuwa nyekundu kuliko kawaida
  • Titi kuwa na joto zaidi
  •  Na wakati mwingine usaha kuanza kutoka

BAADHI YA SABABU ZA TITI LAKO KUTOA DAMU NI PAMOJA NA;

1. Maambukizi ya kwenye tissues za ziwa au titi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Mastitis

2. Tatizo la kupata cracks au mpasuko kwenye chuchu za ziwa lako

3. Tatizo la uvimbe ambao hukua kwenye mirija ya maziwa yaani Intraductal papilloma(in milk ducts)

4. Kuumia kwenye ziwa kwa ajali au kupata majeraha yoyote kama vile kupigwa,kuanguka n.k

5. Kupatwa na tatizo la kansa ya matiti kwa kitalaam hujulikana kama Ductal or lobular breast cancer

6. Kupatwa na ugonjwa kwenye maziwa ambao hujulikana kama pagets diseases.

KUMBUKA; kama una dalili kama hizi wahi hospitalini kwa ajili ya vipimo zaidi pamoja na matibabu,

Kwa sababu matibabu ya kansa katika stage za mwanzoni hutoa matokeo mazuri zaidi ikiwa ni pamoja na kupona kabsa,

Tofauti na ukichelewa sana kupata tiba.

Kujua SABABU za Chuchu Kutoa MAZIWA yenyewe SOMA HAPA..!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.