Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA BELL’S PALSY(chanzo,dalili na tiba)

UGONJWA WA BELL’S PALSY(chanzo,dalili na tiba)

Tatizo hili huhusisha mtu kupooza(paralysis) misuli ya usoni na tatizo hili hutokea endapo kuna hitilafu mbali mbali kwenye nerves ambazo zinadhibiti misuli ya usoni kama vile; kuvimba kwa nerves,kubanwa zaidi,n.k

CHANZO CHA TATIZO HILI

– Chanzo cha tatizo hili ni hitilafu ambayo hutokea kwenye nerves ambazo zinadhibiti(control) misuli mbali mbali ya usoni na uharibifu huo ni kama vile kubanwa kwa nerves,kuvimba kwa nerves n.k

Chanzo cha uharibifu huu wa nerves hakijajulikana bado, japo baadhi ya watafiti mbali mbali wa afya wamehusisha tatizo hili pamoja na maambukizi ya Virusi mbali mbali(Viral infections) kama vile;

✓ HIV

✓ herpes simplex

✓ Sarcoidosis

✓ Herpes zoster

✓Epstein- Barr virus

n.k

DALILI ZA TATIZO HILI

– Dalili za tatizo hili huanza kuonekana gafla tu pale mtu unapoamka asubuhi au kujaribu kula na kunywa kitu chochote ndipo unaanza kuona mabadiliko kama vile;

✓ Upande mmoja wa uso wako kushuka chini zaidi na kupinda

✓ Kushindwa kufungua au kufunga jicho moja

✓ Kushindwa kula au kunywa kitu chochote

✓ Mtu kushindwa kucheka

✓ Kupata maumivu makali ya kichwa

✓ Mdomo na jicho kukauka sana

✓ Misuli ya usoni kulegea

✓ N.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

– Tatizo hili huisha lenyewe bila matibabu ndani ya wiki kadhaa au miezi kadhaa, japo mgonjwa huweza kupewa matibabu mbali mbali kama vile; Dawa za maumivu kama Ibuprofen, Dawa jamii ya Corticosteriods kuzuia uvimbe na dawa mbali mbali kwa ajili ya mashambulizi ya virusi yaani Antiviral drugs

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.