Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA MWANAUME KUZALIWA NA CHROMOSOME ZILIZOZIDI KWENYE MBEGU ZAKE ZA KIUME(Klinefelter syndrome)

 Klinefelter syndrome

• • • • •

UGONJWA WA MWANAUME KUZALIWA NA CHROMOSOME ZILIZOZIDI KWENYE MBEGU ZAKE ZA KIUME(Klinefelter syndrome)


Klinefelter syndrome hili ni tatatizo ambalo huhusisha mwanaume kuzaliwa na idadi ya Chromosome zilizozidi kwenye mbegu zake za kiume yaani;


Badala ya mbegu za kiume kubeba Chromosome XY  kama kawaida, Huwa na Idadi ya chromosome X zilizozidi yaani XXY.


XY- Hii ni kawaida kwa mbegu ya Kiume kubeba Chromosome hizi.


XXY- Hili ni tatizo la Klinefelter syndrome


DALILI ZA MWANAUME MWENYE TATIZO LA KLINEFELTER SYNDROME


– Kwa mtoto mdogo jinsia ya kiume huanza kuonyesha dalili mbali mbali kama vile;


• Mtoto Kudhoofika sana kwa misuli yake ya mwili


• Mtoto Kuchelewa kukaa,kutambaa, kutembea,kuongea N.k


• Mtoto kuwa na tatizo la korodani kutokushuka chini kama kawaida


– Mwanaume kuchelewa kubalehe au kutokubalehe kabsa


– Mwanaume kuwa na miguu mirefu zaidi


– Mwanaume kuonyesha mabadiliko madogo sana ya mwili yanayotakiwa kutokea katika kipindi cha ukuaji wa mwili au balehe


– Mwanaume kuwa na matiti kama mwanamke


– Mwanaume kuwa na korodani ndogo sana kuliko kawaida


– Mwanaume kuwa na uume mdogo sana kupita kawaida


– Mwanaume kuwa na hips


– Mwanaume kuwa na nywele chache sana maeneo mbali mbali ya mwili wake kama vile; sehemu za siri


– Mwanaume kuwa na tatizo la kuzalisha mbegu chache sana kuliko kawaida yaani Low sperm count au kuwa na tatizo la kutokuzalisha kabsa mbegu za kiume


MATIBABU YA TATIZO HILI


✓ Hakuna tiba ya kuondoa hizi chromosome zilizozidi(XXY),bali kuna matibabu mbali mbali kwa ajili ya kudhibiti dalili ambazo husababishwa na tatizo hili.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.