Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MWANAMKE MJAMZITO KUPATA UJAUZITO MWINGINE kwa wakati mmoja(superfetation)

 superfetation

• • • • • •

MWANAMKE MJAMZITO KUPATA UJAUZITO MWINGINE kwa wakati mmoja(superfetation)


Bila shaka unaweza kushangaa,ila ukweli ni kwamba mwanamke mjamzito huweza kubeba mimba nyingine wakati huo huo akiwa tayari ni mjamzito kitaalam tunaita Superfetation


Ingawa ni mara chache sana kutokea kwa binadamu, Hali hii hutokea sana kwa wanyama,


Kinachotokea ni kwamba, mwanamke baada ya kupata ujauzito wa kwanza, mimba hujishikiza kwenye mji wa mimba, na wakati huo huo akaendelea kufanya mapenzi eidha na mume wake huyo huyo au na mtu mwingine,


Kisha yai lingine likafanikiwa kurutubishwa na ujauzito mwingine kutokea,


Watoto hawa huzaliwa wakati mmoja kama mapacha,ila ukweli ni kwamba wanatofautiana kidogo sana kwenye Umri,


Endapo mama kashiriki tendo la ndoa na Mwanaume mmoja basi watoto hawa huwa wa baba mmoja,lakini kama mwanamke alifanya mapenzi na wanaume wawili tofauti,tunaweza kupata watoto wawili ambao huzaliwa kwa wakati mmoja kama mapacha ila kila mmoja ana Baba ake.


JE KUNA MADHARA YOYOTE?


– Madhara ni kwamba, ujauzito wa pili kuingia unatofautiana na wakwanza ambapo hata itakapofikia wakati wa kujifungua,kuna uwezekano mkubwa mtoto wa kwanza akazaliwa vizuri na mwingine wa pili kuzaliwa kabla ya wakati yaani premature,


ambapo huweza kupata matatizo mbali mbali kama vile;


✓ Kuzaliwa na uzito mdogo sana


✓ Kupata shida ya upumuaji


✓ mwili kudhoofika sana na kukosa nguvu


✓ Kuwa na shida katika kunyonya maziwa ya mama


✓ kupatwa na tatizo la damu kuvuja kwenye Ubongo


✓ Na mama mjamzito mwenyewe kupatwa na madhara mbali mbali kama vile;


• Kupatwa na kifafa cha mimba


• Kupatwa na kisukari cha ujauzito yaani Gestational Diabetes N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.