Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA UVIMBE NYUMA YA GOTI(Baker’s cyst)

  BAKER CYST

• • • • •

TATIZO LA UVIMBE NYUMA YA GOTI(Baker’s cyst)


Tatizo hili huhusisha maji kujikusanya na kutengeneza kiuvimbe nyuma ya goti(angalia picha hapo chini), hali ambayo hupelekea mtu kupata maumivu makali wakati wa kukunja goti au kunyoosha,


DALILI ZA BAKER’S CYST


– Kupata maumivu makali wakati wa kukunja au kunyoosha goti


– Uvimbe kutokea nyuma ya goti kama kwenye picha hapo chini


– Misuli ya Mguu kukakamaa sana


CHANZO CHA TATIZO HILI


Tatizo hili hutokea pale ambapo  maji ndani ya goti au kwa kitaalam Synovial fluid kujikusanya sehemu moja ya nyuma ya goti kutokana na sababu mbali mbali kama vile;


✓ Mtu kuumia kwenye goti


✓ Maambukizi ya magonjwa kwenye goti


✓ Tatizo la Arthritis


VIPIMO;


Kabla ya kuanza tiba,Mgonjwa huweza kufanyiwa vipimo mbali mbali kama vile;


• Kipimo cha Damu


• Kipimo cha X-RAY


• Kipimo cha ULTRASOUND

N.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


– Zipo njia mbali mbali katika kutibu tatizo hili kutokana na chanzo chake kama vile;


• Mgonjwa kufanyiwa mazoezi maalum ya kusambaratisha huo uvimbe


• Matumizi ya dawa


• Maji ya Synovial fluid ambayo yamejikusanya sehemu moja kuvutwa

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.