Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA SILIKOSISI YA MUDA MREFU (CHRONIC SILICOSIS)

SILIKOSISI YA MUDA MREFU (CHRONIC SILICOSIS)

Mgonjwa mwenye tatizo hili la Chronic silicosis huvuta chembechembe za silika kwa muda mrefu yaani Zaidi ya miaka 10-30 kabla ya kuanza kupata dalili za mwanzo. Mgonjwa akifikia hapa anakua ameshaharibikiwa mapafu yake kwani yatakua na makovu makubwa makubwa na vinundunundu vikubwa vikubwa. Kwa kua hali hii huchukua muda mrefu kutokea basi wagonjwa wengi wanakua wameshastaafu maeneo yao ya kazi au wanakaribia kustaafu.

DALILI ZA UGONJWA HUU WA SILIKOSIS YA MUDA MREFU

Kwa ugonjwa huu watu wengi wanaweza kutokuonyesha dalili yoyote au wakawa na dalili ya kikohozi chenye makohozi tu;aidha dalili zingine ambazo zinaweza kutokea ni kifua kubana,kushindwa kuhema,kifua kuuma ,mwili kuchoka choka na kupungua uzito. Kwa hiyo kama mtu ana historia ya kufanya kazi katika maeneo yenye silika na akawa na dalili hizi basi anaweza akawa na ugonjwa huu.

NAMNA SILIKOSISI YA MUDA MREFU HUGUNDULIKA

Ugonjwa huu hugundulika kupitia historia ya mgonjwa ya kufanya kazi katika maeneo yenye silika,kifua kupimwa na daktari Pamoja na vipimo vya kifua kama x-ray,PET SCAN,Lung biopsy;CT scan au bronchoscopy.

MATIBABU YA SILIKOSISI YA MUDA MREFU

Mpaka ninavyoandika Makala hii hakuna TIBA madhubuti ya hali hii na hivo basi cha kufanya ni KUKWEPA KABISA MAENEO YENYE SILIKA (COMPLETE AVOIDANCE OF FURTHER EXPOSURE); kadhalika mgonjwa hupata matibabu ya kumsaidia kutokana na hali aliyokuja nayo(supportive care). UPANDIKIZAJI WA MAPAFU ndo tiba yenye matunda pekee kwa watu ambao wanazidi kuzidiwa au mapafu kuharibika.

HATMA YA SILIKOSISI YA MUDA MREFU

Wagonjwa wenye hali hii hua wanapata madhara makubwa kwenye mapafu yao kama kuwa na makovu makubwa na manundu manundu hivo basi miaka ya kuishi hupungua kwa miaka 9-14.

KUJIKINGA NA HALI HII

Kuwepo na njia Madhubuti kwa ajili ya kuwalinda wafanyakazi waliopo kwenye maeneo yenye silika kama vizuia mavumbi au chembe chembe za silika ili zisiingie kwenye mapafu ya mfanyakazi. Vile vile ni kuacha KUVUTA SIGARA AU MOSHI WA SIGARA KABISA; MUHIMU SANA Hii..

SILIKOSISI MWENDOKASI (ACCELERATED SILICOSIS)

katika aina hii mgonjwa atapata dalili za ugonjwa huu ndani ya miaka 10 na ni dalili ambazo hujitokeza harakaharaka na zinaleta madhara haraka haraka ikiwemo kupoteza Maisha.Ugonjwa huu tofauti yake na aina zingine ni kwamba mtu huanza kuumwa ndani ya kipindi cha miaka 10, mgonjwa anaweza asipate dalili yoyote na hali hii inaweza kuonekana kweye x ray ya kifua tu. Matibabu na namna ya kujilinda ni kama aina zingine hapo juu

MAGONJWA YANAYOAMBATANA NA WATU WENYE TATIZO LA SILIKOSISI

Yapo baadhi ya magonjwa ambayo Pamoja na mgonjwa kua na silikosisi anakua na magonjwa mengine ambayo kwa Pamoja yanazidi kudhoofisha afya ya mgonjwa na kupunguza umri wa mgonjwa kuishi; magonjwa hayo ni kama vile;

1)Kifua kikuu (tuberculosis (TB))

2)Magonjwa ya figo ikiwemo tatizo la figo kufeli(Chronic kidney disease&kidney failure)

3)Saratani ya mapafu (Lung cancer)

4)Ugonjwa wa sakaoidi (Sarcoidosis)

5)Magonjwa ya rumatiki (Rheumatic disease)

6)Maambukizi ya sumu kuvu ya aspergila kwenye mapafu(Chronic necrotizing aspergillosis)

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.