Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA INI LITOKANALO NA UNYWAJI POMBE KUPITA KIASI

FAHAMU KUHUSIANA NA TATIZO LA INI LITOKANALO NA UNYWAJI POMBE KUPITA KIASI.

Unywaji sugu na uliopitiliza wa pombe ni moja ya sababu kuu za matatizo ya ini. Pombe ina athiri ini katika viwango mbalimbali na asilimia chache hufikia hatua ya mwisho kabisa ya kuharibika kwa ini. Idadi ya unywaji, vyakula, uzito uliopitiliza pamoja na jinsia vinahusika moja kwa moja katika kuamua au kupelekea hatua za uharibifu huo.

Pombe ni kihatarishi namba tatu duniani katika kusababisha magonjwa mbalimbali. Na matumizi yasiyosahihi ya pombe yanasababisha vifo zaidi ya milioni 2.5 kila mwaka duniani kote.

NAMNA/JINSI AMBAVYO POMBE HUATHIRI INI PAMOJA NA SABABU ZAKE.

Kiwango na muda ambao mtu ametumia pombe ndivyo vihatarishi vikuu vya tatizo hili. Wanawake wapo katika hatari zaidi ya kuharibika kwa ini kutokanako na pombe ukilinganisha na wanaume.

Japokuwa sababu hazifahamiki vizuri, homoni ya estrogen, kiwango cha mafuta katika mwili, na uchakatwaji wa pombe katika mfumo wa chakula wa mwanamke kunaongeza hatari ya tatizo hili.
Muda ambao huchukua mpaka kuharibika kwa ini unategemea pia kiwango cha pombe ambacho mtu hunywa.

Uzito uliopitiliza, ulaji wa vyakula vyenye mafuta pamoja na matumizi ya kahawa huchochea mabadiliko ya ini yatokanayo na pombe.

Maambukizi sugu ya virusi vya hepatitis C ni miongoni mwa matatizo ambatano ambayo huchochea kuharibika zaidi kwa ini kutokanako na pombe hasa kwa wanywaji sugu.

Inaaminika kuwa pombe huathiri ini moja kwa moja yaani huwa kama sumu kwenye ini. Unywaji wa pombe huanzisha matokeo ya inflamasheni ambayo hudhuru seli za ini kwa namna mbalimbali. Sumu mbalimbali ikiwemo zile zitokazo katika mfumo wa chakula hupelekea kufa kwa seli za ini.

Matokeo mengine ya inflamesheni huamsha mfumo kinga wa mwili ambao pia huweza changia kuharibika kwa ini zaidi. Kufa kwa seli za ini kuambatanako na kushindwa kutengenezwa kwa seli nyingine kunapelekea kuamshwa kwa seli zifahamikazo kama stellate na kutengenezwa kwa collagen ambazo hupelekea mabadiliko katika maumbile ya ini.

Unywapo pombe kunapelekea kukusanyika kwa mafuta mafuta katika maeneo mbalimbali ya ini, hasa kwenye sehemu ambako kichocheo kiitwacho alcohol dehydrogenase hupatikana.

Unywapo pombe kunapelekea kukusanyika kwa mafuta mafuta katika maeneo mbalimbali ya ini, hasa kwenye sehemu ambako kichocheo kiitwacho alcohol dehydrogenase hupatikana. Yote haya hupelekea kuharibika kwa mfumo, muonekano pamoja na maumbile ya ini.

DALILI ZAKE NI PAMOJA NA;

1. Kuongezeka kwa ukubwa wa ini.

2. Maumivu ya tumbo hasa upande wa kulia wa juu wa tumbo.

3. Kichefuchefu

4. Manjano

5. Homa

6. Tumbo kujaa maji

7. Kuvuja damu nk

Dalili hizi hutegemea na hatua ya ugonjwa.

MATIBABU YA TATIZO HILI

ziko dawa hutumika katika kutibu tatizo hili iwapo lipo katika hatua flani. Lakini Tiba kuu ni KUACHA POMBE.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.