Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA KUKOSA CHOO KWA MTU MZIMA

TATIZO LA KUKOSA CHOO KWA MTU MZIMA

Tatizo hili la mtu kukosa choo huwapata watu wengi na kwa asilimia kubwa huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile mtu kupata choo kigumu sana pale anapofanikiwa kupata choo,maumivu wakati wa kujisaidia n.k

Kuna matatizo mbali mbali yanayohusiana na mfumo mzima wa haja kubwa,na matatizo hayo ni kama vile; Mtu kujisaidia choo kigumu sana yaani Constipation,mtu kukosa kabsa choo kwa muda flani,mtu kujisaidia haja kubwa ambayo imechanganyika na damu, mtu kuharisha, n.k, Matatizo haya yote kwa ujumla wake yanachangiwa na sababu ambazo kwa kiasi kikubwa zinaingiliana.

Swali,je mtu kukosa choo ni ugonjwa au tatizo? Ndiyo ni tatizo, kwa binadamu mwenye afya njema lazima apate choo kila siku angalau mara moja kwa siku na kama anakula chakula na ashiba vizuri huweza kujisaidia kuanzia mara 2 mpaka 3 kwa siku, Hivo mtu kukaaa kwa siku nzima bila kujisaidia sio afya bali ni tatizo, na hapa chini tumechambua baadhi ya sababu za tatizo hilo;

SABABU ZA MTU KUKOSA CHOO NI PAMOJA NA;

1. Kutokula chakula kabsa

2. Matatizo ya kuziba kwa njia ya haja kubwa kutokana na sababu mbali mbali kama vile uvimbe n.k

3. Matatizo kwenye kibofu cha mkojo kama vile tatizo la Chronic kidney failure

4. Ugonjwa wa kisukari

5. Tatizo la Hypothyroidism

6. Matatizo kwenye mfumo wa nerves yaani Neurologic disorders kama vile; Ugonjwa wa Parkinson’s, Multiple sclerosis n.k

7. Mtu kuumia kwenye mfumo wa uti wa mgongo yaani Spinal cord injury

8. Kupatwa na tatizo la Saratani ya utumbo mpana(Colon cancer) au Saratani ya kwenye njia ya haja kubwa kama vile Rectal cancer n.k

9. Mtu kutokunywa maji ya kutosha kila siku,unashauriwa kunywa maji angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa siku

10. Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; Dawa jamii ya anticonvulsants,antidepressants,dawa za magonjwa ya moyo kama vile Calcium channel Blockers, dawa za kutuliza maumivu kama vile Codeine,Morphine n.k

KUMBUKA; Mtu mwenye tatizo hili la kukosa choo huweza kupatwa na matatizo mengine kama vile;

– Tumbo kujaa gesi mara kwa mara

– Tumbo kuwa kubwa zaidi au kuongezeka size

– Kukosa kabsa hamu ya chakula

– Kupatwa na maumivu ya Tumbo mara kwa mara

– Kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu,siku akibahatika kujisaidia n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.