Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA SCLEROMYXEDEMA,CHANZO NA TIBA

UGONJWA WA SCLEROMYXEDEMA,CHANZO,DALILI NA TIBA

Huu ni ugonjwa ambao huhusisha ngozi ya Binadamu kuwa na manundu manundu pamoja na mikunjo kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wa binadamu,ugonjwa huu ulianza kwenye miaka ya 1905,

Maeneo ambayo huathiriwa sana na tatizo hili ni pamoja na, paji la uso,shingoni,mikononi,miguuni na kwenye mapaja.

Ugonjwa huu huwapata sana watu wenye umri wa kati ya miaka 30 na 50

CHANZO CHA UGONJWA WA SCLEROMYXEDEMA

– Chanzo halisi bado hakijulikani, japo baadhi ya tafiti zimehusisha ugonjwa huu pamoja na tatizo la Kansa au Saratani kwenye Mifupa yaani Bone marrow Cancer kama vile; Myeloma,Lymphoma,Leukemia n.k

DALILI ZA UGONJWA WA SCLEROMYXEDEMA NI PAMOJA NA;

• Ngozi ya Binadamu kuwa na manundu manundu pamoja na mikunjo kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wa binadamu kama vile; kwenye paji la uso,shingoni,mikononi,miguuni na kwenye mapaja.

• Pia ugonjwa huu huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile;

– Kushindwa kusinyaa kwa misuli ambayo inasaidia mtu kumeza kitu tatizo ambalo hujulikana kama Esophageal aperistalsis

– Mtu kupatwa na matatizo ya macho yaani Eye abnormalities

– Mtu kushindwa kupumua vizuri n.k

MATIBABU YA UGONJWA WA SCLEROMYXEDEMA

✓ Kuna huduma mbali mbali za kimatibabu kwa mtu mwenye tatizo hili ikiwemo;

• Mgonjwa kupata dawa za Intravenous Immunoglobilin(IVIG)

• Plasmaphereis kama matibabu ya muda mfupi yaani short-term

• Mgonjwa kupewa Thalidomide pamoja na Systemic Glucocorticoids, N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.