Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA HATARI KWA MAMA MJAMZITO

Ziko dalili nyingi ambazo zinaweza kumpata mama mjamzito na iwapo utaona dalili hizi ni vyema ukafika katika kituo cha kutolea huduma mapema iwezekanavyo.

Ziko jamii za watu ambazo zimekuwa zikichukulia dalili hizi kama hali ya kawaida na wengine wamekuwa wakijitibia nyumbani pasipo kujua madhara yanayoweza kutokea iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa. Miongoni mwa dalili hizi ni pamoja na;

1. Mama mjamzito Kuishiwa nguvu au kushindwa/kukosa nguvu za kutoka kitandani

2. Changamoto ya upumuaji (kuhema haraka haraka au kukosa pumzi)

3. Dalili zote za Degedege

4. Dalili zote za kifafa cha mimba kama vile;

– mjamzito kuona marue rue

– mjamzito kuvimba sana miguu,mikono na uso

– mjamzito kuumwa sana na kichwa

– presha kuwa juu sana pamoja na uwepo wa protein kwenye mkojo n.k

5. Homa kali au joto la mwili kuwa juu sana

6. Maumivu makali ya tumbo

7. Kupungua kwa kucheza kwa mtoto tumboni kusiko kwa kawaida. Au mtoto kuacha kucheza kabisa.

8.Chupa ya uzazi kupasuka kabla ya wakati yaani premature rupture of membrane

8. Maumivu makali ya kichwa na nuru hafifu

9. Kutokwa na damu ukeni

10. Kuvimba vidole, uso na miguu sana

11. Kutapika sana na kukosa hamu ya kula

N.K

Kila mama mjamzito pamoja na mwenza wake wana haki ya kupata elimu juu ya dalili hizi na iwapo wataziona basi ni vyema wakafika katika kituo cha afya ili kuokoa maisha ya mtoto tumboni pamoja na maisha ya mama mjamzito.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.