Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

BAADHI YA WANAWAKE KUPATWA NA SHIDA YA MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI(peripartum cardiomyopathy)

BAADHI YA WANAWAKE KUPATWA NA SHIDA YA MOYO KUSHINDWA KUFANYA KAZI(peripartum cardiomyopathy)

Mwezi mmoja kabla ya kujifungua na miezi kadhaa baada ya kujifungua ndani ya miezi 5) asilimia chache ya wanawake
hupata shida ya moyo kushindwa kufanya
kazi kitaalamu huitwa “peripartum
cardiomyopathy”

Japokuwa tatizo hili ni nadra, asilimia kadhaa ya wanwake wamekuwa wakipata shida ya moyo kushindwa kufanya kazi katika kipindi cha mwezi mmoja kabla ya kujifungua na ndani ya miezi mitano baada ya kujifungua.

Tatizo ili hutofautishwa na shida nyingine kwa sifa zake, nazo ni;

1. Kutokea kwa shida hii kipindi cha mwisho wa ujauzito na miezi ya awali baada ya kujifungua

2. Kipimo cha ECHO kuonesha kupungua kwa kiwango cha damu kinachotolewa/kusukumwa na moyo kwa chini ya asilimia 45.

3. Kutokuwepo kwa sababu yoyote ambayo inaweza husishwa na dalili atakazokuwa nazo mgonjwa

4. Kutokuwa na shida ya moyo kabla.

Baadhi ya tafiti zinaonesha kuwa homoni katika nyakati za mwisho za ujauzito hutengeneza mazingira haribifu (sumu) katika mishipa ya damu ambayo hupelekea shida hii.

Kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin hutolewa na tezi ya pituitary na huvunjwa vunjwa na kutengeneza sumu zinazoharibi mishipa ya damu, kutengeneza vianzilishi vya inflamesheni na utengenezaji wa kemikali.

Pia kondo la nyuma hutengeneza kemikali ambayo hushirikiana na kemikali itokanayo na homoni ya prolactin zinahusishwa kusababisha tatizo hili.

Sababu nyingine ni inflamesheni, virusi, kurithi, muitiko usiosahihi wa kinga ya mwili nk.

Miongoni mwa vihatarishi Vinavyousishwa na nzao nyingi mimba yenye watoto mapacha, umri mkubwa, shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito, nk.

Miongoni mwa vipimo vinavyofanyika ni ECHO, ECG, MRI, na vipimo vya maabara.

Katika tafiti zilivyofanyika zinaonesha tatizo kuonekana zaid nchini nigeria na togo na ni miongoni mwa matatizo yanayohatarisha maisha.

Miongoni mwa dalili ni Kukosa pumzi (hewa), kukosa pumzi hasa unapofanya kazi, kuchoka, kuvimba miguu, kifua kubana nk

Uonapo dalili wahi hospitali maana inawezekana dalili hizi zikawa ni tatizo hili lakini pia inawezekana ni tatizo jingine ambalo linaweza fanania na hili. Matibabu hufanyika hospital kwa dawa na hata okisijeni iwapo itahitajika.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.