Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

VISABABISHI VYA TATIZO LA KUTOKWA UCHAFU UKENI

VISABABISHI VYA TATIZO LA KUTOKWA UCHAFU UKENI

Sababu za kutokwa na uchafu ukeni huhusisha vyanzo vingi sana,na baadhi ya vyanzo hivo ni pamoja na;

1. BACTERIA VAGINOSIS

Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi,kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano wa kawaida katika mazingira ya uke,

wanawake wenye wapenzi wengi na wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari zaidi ya kupata tatizo hili

2. TRICHOMONAS

Maambukizi haya hutokana na Aina ya protozoa wa seli moja, trichomonas mara nyingi huambukizwa kwa njia ya ngono,

protozoa huyo huweza kukaa kwenye unyevu unyevu kwa Muda wa saa 24 Bila kufa hivyo kufanya taulo na chupi zisizokauka kuwa chanzo kingine cha tatizo hili

3. FUNGAL OR YEAST INFECTION

Kwa kawaida Kuna kiwango kidogo cha yeast (candida albicans) katika uke, huwa tunasema Kuna maambukizi pale kiwango kinapozidi Hali ambayo inatokana na kubadilika kwa Hali ya hewa ukeni (Change in the PH balance of vagina)

Maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ndoa au hayapo kwenye kundi la magonjwa ya zinaa yaani sexual transmitted diseases(STD’s).

Mambo ambayo huchangia tatizo hili ni pamoja na:

– Mwanamke kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri au zenye unyevu unyevu mara kwa mara,

hivo kutengeneza mazingira mazuri ya Fangasi kuzaliana kwa wingi

– Mwanamke kuwa na tabia ya kushare taulo za kuogea na watu wengine

– Mwanamke kuwa mchafu,kutokuoga,kutonyoa nywele za sehemu za siri, n.k

– Mwanamke kuvaa nguo za ndani chafu kwa muda mrefu

– Mwanamke kutojisafisha vizuri au kutokubadilisha Pedi wakati wa hedhi n.k

4. VAGINAL OR CERVICAL CANCER,

Kuwa na saratani ya uke(vaginal cancer) au saratani ya mlango wa kizazi(cervical cancer) huweza kuchangia tatizo la kutokwa na uchafu ukeni

Mwanamke anapokua na kansa ya uke au kansa ya mlango wa kizazi huweza kutokwa na maji yenye harufu mbaya,

hivyo ni heri uwe unafanya check up ili kujua Afya yako na kwakuwa cancer ya kizazi inapona hivyo ni vema ukatambua mapema uanze tiba

5. SEXUAL TRANSMITTED DISEASES(STDs)

Kuna baadhi ya magonjwa kama vile KASWENDE NA KISONONO yanasababishwa na ngono na kuwa chanzo cha tatizo hili.

6. POOR HYGIENE
Tatizo la kutokwa na maji wakati mwingine husababishwa na mhusika kua mchafu yani mtu unaoga kwa siku mara moja, chupi moja ndio hiyo hiyo mwaka mzima, pads unakaa nayo saa 24, ukienda kukojoa ujitawadhi na maji masafi hivyo unategemea utakua salama kweli??? Zingatia usafi wa mwili pia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.