Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

KUTOKWA NA DAMU WAKATI WA UJAUZITO

KUTOKWA NA DAMU WAKATI WA UJAUZITO

Kuna sababu nyingi huweza kuchangia tatizo la mwanamke kuvuja damu wakati wa ujauzito ambazo zingine zinahitaji msaada wa haraka sana kwani ni hatari.

DAMU KUVUJA KWENYE MIEZI 3 YA KWANZA YA UJAUZITO(1st trimester)

Baadhi ya sababu za damu kuvuja kwenye kipindi hiki ni pamoja na:

– Tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi yaani kwa kitaalam Ectopic pregnancy

– Kuvuja damu wakati kijusi kikijishikiza kwenye mji wa mimba yaani Implantation bleeding,

ambapo mara nyingi huanza kutokea kwenye siku 10 mpaka 14 baada ya kubeba mimba

– Tatizo la mimba kutoka yenyewe kabla ya wiki 20 yaani Miscarriage

– Tatizo la Molar pregnancy ambapo yai lililorutubishwa hubadilika na kuwa abnormal tissue badala ya mtoto

– Matatizo mbali mbali kwenye mlango wa kizazi au cervix, kama vile;

Maambukizi kwenye mlango wa kizazi(cervical infection), kukuwa kwa nyama kwenye mlango wa kizazi au (inflamed cervix or growths on the cervix)

DAMU KUVUJA KWENYE MIEZI 3 YA PILI NA TATU YA UJAUZITO( 2nd or 3rd trimester)

Baadhi ya sababu za damu kuvuja kwenye kipindi hiki ni pamoja na:

– Tatizo la mlango wa kizazi kushindwa kuhimili ujauzito na kuanza kufunguka kabla ya wakati(Incompetent cervix-a premature opening of the cervix, which can lead to preterm birth)

– Tatizo la mimba kutoka yenyewe kabla ya wiki 20 yaani Miscarriage,

– Tatizo la mtoto kufia tumboni au intrauterine fetal death

– Tatizo la kondo la nyuma kuachia sehemu ya kujishikiza yaani Placental abruption

– Tatizo la kondo la nyuma kushuka na kuziba mlango wa kizazi yaani Placenta previa, huweza kusababisha pia mwanamke kuvuja damu nyingi wakati wa ujauzito

– Tatizo la Mwanamke kuanza kupata uchungu kabla ya wakati yaani Preterm labor,

– Matatizo mbali mbali kwenye mlango wa kizazi au cervix, kama vile;

Maambukizi kwenye mlango wa kizazi(cervical infection), kukuwa kwa nyama kwenye mlango wa kizazi au (inflamed cervix or growths on the cervix)

– Tatizo la kupasuka kizazi yaani Uterine rupture hasa kwa mwanamke ambaye hapo kabla aliwahi kujifungua kwa upasuaji

– Kuvuja damu wakati wa ujauzito baada ya kupigwa au kuanguka na kuumia n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.