Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MATIBABU YA CHUNUSI

MATIBABU YA CHUNUSI

Matibabu ya chunusi yapo na yanaweza kuchukua muda wa miezi 2 hadi 6 ya kutumia dawa pamoja na kubadili mtindo wa maisha. Katika matibabu ya chunusi ni lazima mgonjwa azingatie mambo yafuatayo

Mtu mwenye chunusi ni lazima akwepe mambo yafuatayo

1)Epuka kabisa kula vyakula vya mafuta mengi,epuka kabisa kula kuku wa kisasa na nyama nyekundu

2)Epuka kutumia maziwa mara kwa mara au bidhaa za maziwa mara kwa mara

3)Epuka kabisa kujikuna,kujibinya binya usoni (Avoid picking of acne lesions)

4)Epuka kutumia mafuta,lotion,cream au bidhaa yeyote ya ngozi zenye kemikali zinazoleta chunusi (Select noncomedogenic skin care and cosmetic products)

5)Epuka kusugua sugua usoni au sehemu zenye chunusi kwa kutumia vitu vigumu vigumu,vitambaa vigumu,kemikali kali zinazochomachoma usoni (Utilize gentle skin cleansers rather than soaps or scrubs)

6)Epuka sana kufanya scrub mara kwa mara za kutumia nguvu yaani misuguano ya nguvu sana (Avoid aggressive scrubbing of the skin)

Baada ya mgonjwa kutambua na kubadilika kuacha mambo tajwa hapo juu basi mamabo kadhaa hutazamwa kabla ya matibabu ya chunusi.

Yapo madawa mbali mbali ya chunusi kama za kumeza na kupaka na madawa haya hutolewa kwa kuangalia;

• aina ya chunusi aliyonayo mgonjwa

• aina ya ngozi

• umri na hali ya mgonjwa ,

kama mgonjwa alishawahi kutumia dawa au la na kama chunusi zishaleta madhara au la na madhara yapi na yapi yametokea.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.