Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA WATOTO WENYE TATIZO LA USONJI

DALILI ZA WATOTO WENYE TATIZO LA USONJI NI PAMOJA NA;

– Mtoto kushindwa kuitika baada ya kuitwa jina lake au mtoto kuonekana kutokusikia kabsa wakati akiitwa jina lake

– Mtoto kushindwa kutazama watu usoni(eye contacts), kutokucheka,n.k

– Mtoto kutokuongea kabsa au kuchelewa sana kuongea kuliko kawaida

– Kupoteza uwezo wa kutamka maneno au sentensi ambazo mwanzoni alikuwa anaweza kutamka

– Mtoto kushindwa kabsa kuanzisha mazungumzo

– Mtoto kuongea huku akitoa sauti zisizozakawaida

– Mtoto kushindwa kuelewa maswali rahisi akiulizwa na watu

– Mtoto kufanya vitu vya kujidhuru mwenyewe kama vile; kujipiga mwenyewe,kujibamiza kichwa n.k

– Mtoto kutokutaka mwanga,kushtuka sana akiguswa au kusikia sauti yoyote

– Mtoto kutokutamka maneno ya kitoto mpaka afikishe umri wa mwaka mmoja na kuendelea

– Mtoto kutokuongea neno lolote mpaka afikishe kipindi cha umri wa miezi kumi na sita

– Mtoto kupoteza kabsa uwezo wake wa kuongea

– Mtoto kushindwa kufanya vitu mbali mbali kama kupunga mkono kwa wazazi au mtu yoyote kama ishara ya kumsalimia au kumuaga mpaka anapofikisha kipindi cha umri wa miezi kumi na mbili

– Mtoto kushindwa kuongea maneno zaidi ya mawili au sentensi ya maneno mpaka anapofikisha umri wa miezi 24

– Mtoto kuwa na tabia ya kukaa peke yake pamoja na kujitenga na watu N.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.