Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DAWA YA FUNGUS SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE

DAWA YA FUNGUS SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE

Dawa ya fangasi ukeni ya vidonge vya kudumbukiza yaani kwa kitaalam hujulikana kama vaginal suppositories, Pamoja na dawa zingine kwenye forms tofauti huweza kutumika kutibu tatizo la Fangasi Ukeni.

Zipo dawa nyingi ambazo hutumika katika matibabu ya Fangasi ukeni,huku zingine zikiwa za asili na zingine za hospital. Lakini kwa upande wangu nitaelezea baadhi ya dawa za hospital zinazotumika kutibu tatizo la Fangasi ukeni.

NB; Fangasi jamii ya Candida albicans ndiyo hushambulia sana sehemu za siri za mwanamke.

DALILI ZA FANGASI UKENI NI PAMOJA NA;

1. Mwanamke kupata miwasho sehemu za siri ikiwa ni pamoja na eneo la ngozi kati ya njia ya haja kubwa na sehemu za siri

2. Mwanamke kutokwa na uchafu wenye rangi kama maziwa,ambao huambatana na harufu mbaya ukeni

3. Sehemu za siri kuwa na michubuko pamoja na vidonda kwenye mashavu na ngozi ya ukeni

4. Ngozi ya sehemu za siri kubadilika rangi na kuwa nyekundu

5. Kupata maumivu wakati wa tendo la Ndoa

MADHARA YA FANGASI WA UKENI NI PAMOJA NA;

– Mwanamke kuwa na harufu au kutoa harufu mbaya sehemu zake za siri

– Mwanamke kutokwa na uchafu mithili ya maziwa Mgando

– Mwanamke kuwa mkavu na Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa

– Sehemu za siri za mwanamke kuwa na michubuko pamoja na vidonda

– Kukosa raha ya tendo la Ndoa

– Kukerwa na miwasho sehemu za siri hata ukiwa mbele za watu

– Fangasi sugu huweza kukusababishia hata tatizo la kutokushika mimba

DAWA YA FUNGUS SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE

• Baadhi ya Dawa ambazo hutumika hospitalini kutibu tatizo la fangasi ni fluconazole,Clotrimazole pamoja na dawa nyingine nyingi,

kulingana na dalili za fangasi wa ukeni mwanamke huweza kushauriwa na wataalam wa afya kutumia Clotrimazole ambapo kuna Cream ya kupaka sehemu za siri pamoja na ile ya vidonge vya kudumbukiza ukeni yaani kwa kitaalam vaginal suppositories, ambapo vinaweza kuwa vitatu au sita kulingana na dose yake.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.