Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

KUNYWA MAJI MENGI KUNA FAIDA GANI

KUNYWA MAJI MENGI KUNA FAIDA GANI

?Faida za Kunywa Maji mengi Mwilini Mfano;Wastani wa lita 2.5 kwa siku

– Kunywa Maji mengi hutibu tatizo la Kukosa Choo,pamoja na tatizo la kupata Choo kigumu yaani constipation

– Kunywa maji mengi husaidia kusafisha mwili na Kuondoa Sumu mwilini,hasa kwa Njia ya kukojoa

– Kunywa maji mengi husaidia kutibu magonjwa kama UTI(Urinary Track Infection) au kwa lugha ya Kiswahili ni maambukizi katika Njia ya Mkojo,ambapo tafiti zinaonyesha Unywaji wa maji Wastani wa lita 2.5 kwa siku,hupunguza uwezekano wa kupata UTI za mara kwa mara kwa zaidi ya asilimia 50%

– Unywaji wa maji mengi husaidia pia kutibu matatizo kama Kuumwa na KICHWA

– Kunywa maji mengi husaidia Ngozi ya mwili kunawiri kila wakati

– Unywaji Maji mengi husaidia kuzuia mtu kupatwa na Magonjwa Ya Moyo,Mfano; Utafiti uliofanyika Nchini Marekani kwa kipindi cha Miaka sita,husema kwamba unywaji waji Wastani wa Glasi 5 kila siku,husaidia kumkinga Mtu na magonjwa ya moyo kwa Wastani wa asilimi 41%  zaidi ya wale wanaokunywa Glasi 2 au Chini ya hapa kwa siku

– Unywaji wa Maji mengi husaidia Kuupa Mwili Nguvu na kuondoa Uchovu kabsa.

– Kunywa Maji mengi husaidia kumkinga Mtu na Saratani ya Utumbo,kwani chakula na Usagaji wake utaenda vizuri kama Unakunywa Maji ya kutosha.

➖ KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.