Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA KUVIMBA FIZI(chanzo chake)

TATIZO LA KUVIMBA FIZI(chanzo chake)

Baadhi ya watu hupatwa na tatizo hili la kuvimba Fizi kutokana na Sababu mbali mbali, baadhi ya Sababu hizo ni kama vile;

1. Kuingia kwa particles ndogo ndogo za vyakula kwenye Fizi,

Hii huweza kutokea pale mtu anapokula vitu vigumu au vyenye chembe chembe ngumu kama vile za Popcorns n.k

Particles hizi huweza kuingia ndani ya fizi na kusababisha fizi kuanza kuvimba.

2. Tatizo la Gingivitis ambalo huchangia kwa asilimia kubwa watu kuvimba fizi,

Gingivitis-ni ugonjwa wa Fizi ambao husababisha Fizi kuvimba, na chanzo chake kikubwa ni kutokufanya usafi wa kinywa au Poor Oral hygiene.

3. Hali ya Ujauzito, Baadhi ya Wanawake wakiwa wajawazito hupatwa na tatizo hili la FIZI kuvimba,

Chanzo cha Fizi kuvimba Wakati wa Ujauzito ni kutokana na mabadiliko makubwa ya vichocheo vya mwili,hali ambayo hupelekea damu nyingi kuflow kwenye Fizi na kusababisha Fizi kuvimba

4. Maambukizi ya Magonjwa mbali mbali kama Vile Fangasi wa mdomoni(Oral thrush/Yeast),Herpes n.k

Magonjwa haya huweza kusababisha tatizo la kuvimba kwa Fizi.

5. Side effects ya baadhi za Dawa, Baadhi ya dawa huweza kusababisha tatizo la kuvimba kwa Fizi

6. Mtu kuwa na tatizo la Utapiamlo au kwa kitaalam Malnutrion

7. Mtu kuwa na tatizo la Mzio au Allergy kwa baadhi ya vitu kama vile; Baadhi ya Dawa za Meno, Mouthwash, akila nyama n.k

8. Mtu Kuvaa vitu vyovyote kwenye meno kama vile meno bandia ambayo hayafiti vizuri kwenye meno n.k

9. Na baadhi ya Watu huweza kuvimba Fizi baada ya kunywa Pombe au kutumia tumbaku.

KUMBUKA; kama una tatizo hili,Tiba yake hutegemea na chanzo husika, na;

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.