Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI

Zipo faida nyingi sana kwa mtu ambaye anafanya mazoezi mbali mbali ya mwili, unashauriwa kutenga muda angalau wa Nusu saa(dakika 30) kila siku kwa ajili ya kufanya mazoezi ili kuimarisha afya yako.

FAIDA ZA KUFANYA MAZOEZI YA MWILI NI PAMOJA NA;

– Mazoezi husaidia kuzuia tatizo la uzito kupita kiasi yaani Overweight/Obesity,

KUMBUKA: ufanyaji wa mazoezi pamoja na chakula(Diet) ndyo vitu vikubwa sana vya kuzingatia ili kuweka uzito wako wa mwili kuwa sawa.

– Mazoezi husaidia kuimarisha afya yako,Kinga yako ya mwili kuwa imara pamoja na kukukinga na magonjwa mbali mbali kama vile;

• magonjwa ya moyo

• Ugonjwa wa Presha

• Tatizo la kiharusi au STROKE

• Aina mbali mbali za kansa/saratani

• Tatizo la Arthritis

• Ugonjwa wa kisukari(Type 2 diabetes) n.k

– Mazoezi husaidia kuondoa lehemu(Choletrol) pamoja na mafuta mabaya mwilini

– Mazoezi husaidia kuboresha mfumo mzima wa chakula na kuondoa matatizo kwenye mfumo wa umeng’enyaji wa chakula pamoja na matatizo mengine kama vile; Kiungulia(Heartburn), Acid reflux, Metabolic syndrome n.k

– Mazoezi humsaidia mtu kuwa na furaha,kurelax, kuondoa msongo wa mawazo n.k

– Mazoezi husaidia sana kuboresha uwezo wako wa kufikiria ikiwa ni pamoja na kuimarisha afya ya ubongo

– Mazoezi husaidia kuwe na mzunguko mzuri wa damu mwilini

– Mazoezi huimarisha misuli pamoja na viungo mbali mbali vya mwili

– Mazoezi husaidia sana kuboresha afya ya Uzazi

– Mazoezi husaidia sana mtu kupata usingizi mzuri

– Mazoezi huupa mwili nguvu n.k

FANYA MAZOEZI,BORESHA AFYA YAKO

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.