Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

KANSA YA MATITI KWA WANAUME,CHANZO,DALILI NA TIBA

KANSA YA MATITI KWA WANAUME,CHANZO,DALILI NA TIBA

Asilimia kubwa ya watu hawajui kwamba kuna saratani au kansa ya ziwa kwa wanaume,wengi wao wanajua kwamba kuna kansa/saratani ya matiti kwa wanawake tu.

Ila ukweli ni kwamba,hata wanaume huweza kupatwa na aina hii ya saratani japo namba yao sio kubwa kama wanawake.

CHANZO CHA KANSA YA MATITI KWA WANAUME

– Hakuna sababu ya moja kwa moja ambayo hujulikana kama chanzo cha Kansa hii japo kuna baadhi ya vitu ambavyo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata aina hii ya saratani kama vile;

✓ Umri kuwa mkubwa

✓ Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo huhusisha kuongeza vichocheo vya mwilini kwa muda mrefu

✓ Kuwa na historia ya tatizo hili katika famili yenu

✓ Mwanaume kufanyiwa upasuaji wa korodani

✓ Unene kupita kiasi

N.K

Pia kuna utafiti ambao umefanywa “according to new research funded by the charity Breast Cancer Now and published in Breast Cancer Research”

Utafiti huu unasema kwamba ” Wanaume ambao hawana uwezo wa kuzalisha yaani Infertile men wapo kwenye hatari mara mbili ya kupata kansa hii ya matiti kuliko wale ambao hawana matatizo yoyote ya uzazi(fertility issues)”

DALILI ZA KANSA YA MATITI KWA WANAUME NI PAMOJA NA;

– Mwanaume kupata maumivu makali kwenye ziwa

– Mwanaume kuanza kutoa usaha au damu kwenye ziwa

– Ziwa moja kuanza kuwa kubwa kuliko lingine

– Sehemu ya ziwa kubadilika rangi na kuwa nyekundu sana

– N.K

MATIBABU YA KANSA YA MATITI KWA WANAUME

-Mojawapo ya matibabu ya kansa hii ni pamoja na mgonjwa kufanyiwa upasuaji, huduma ya Chemotherapy, dawa za vichocheo mwilini, huduma ya mionzi(Radiation therapy) N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.