Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA HOMA YA NYANI(UGONJWA WA MONKEYPOX)

UGONJWA WA HOMA YA NYANI(UGONJWA WA MONKEYPOX)

Ugonjwa huu unasababishwa na virusi ambao hujulikana kwa jina la MonkeyPox.
Monkeypox Virus wapo kwenye kundi la Orthopoxvirus genus ndani ya familia ya Poxviridae.

Ugonjwa wa homa ya nyani kwa binadamu(Human monkeypox),Mara ya kwanza kabsa uliripotiwa Mwaka 1970 nchini DRC(Democratic Republic of the Congo) kwa kijana mmoja wa Miaka 9 aliyekuwepo kwenye eneo ambalo ugonjwa wa Smallpox ulishaondolewa tangu mwaka 1968. Ndipo visa vingine vikaanza kuripotiwa na maeneo mengine, (Disease history Source:WHO)

DALILI ZA UGONJWA HUU WA MONKEYPOX NI PAMOJA NA;

– Mtu kuwa na homa pamoja na mwili kutetemeka

– Kupata maumivu makali ya kichwa

– Mwili kuchoka kupita kawaida

– Mwili kukosa nguvu na kuwa dhaifu sana

– Lymph nodes kuanza kuvimba ambapo kwa lugha nyingine hujulikana kama lymphadenopathy

– Kupata maumivu ya viungo,joints pamoja na misuli ya mwili

– Kupata maumivu ya mgongo(back ache)

– Kutokewa na UPELE kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wako kama vile; Usoni, kwenye mikono pamoja na viganja vya mikono,
miguuni,machoni,,mdomoni,sehemu za siri n.k

Upele huu unaweza kuwasha sana, na hata baadae huweza kutumbuka kabsa,

Mwili huweza kubaki na makovu au alama alama.

UGONJWA HUU WA HOMA YA NYANI(MONKEYPOX) husambaa kutokana na ukaribu(Close contact) kwa mtu,wanyama au vitu ambavyo tayari vina virusi hawa wa Monkeypox.

Unaweza kuupata kwa njia ya ya mgusano sehemu zenye majeraha, kupitia body fluids zote kama vile damu,mate,jasho n.k, kutoka kwa Mtu au wanyama wenye Virusi hawa(Monkeypox virus).

Virusi vya MonkeyPox vinaweza kuingia mwilini kupitia kwenye ngozi iliyo na jeraha au michubuko yoyote, au kwa njia nyingine kama vile njia ya upumuaji au kupitia macho, pua pamoja na mdomo.

Pia Uenezwaji wake unaweza kuwa  kwa kugusana na wanyama walioambukizwa kama vile nyani, panya na kindi ,kupitia vitu kama vile matandiko au nguo za mgonjwa mwenye virusi hawa.

MATIBABU YA UGONJWA WA MONKEYPOX

Ugonjwa huu hauna tiba(no cure),bali watalaam wa afya hudhibiti dalili zinazotokana na ugonjwa huu wa homa ya nyani.

Hata hivo ugonjwa huu huisha wenyewe kwa kipindi flani baada ya kumpata mtu.

Fahamu pia,Maambukizi haya ya ugonjwa wa homa ya nyani(monkeypox) huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.