Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

BABA NA MAMA KWENDA KLINIKI(MAHUDHURIO)

BABA NA MAMA KWENDA KLINIKI(MAHUDHURIO)

Baba mmoja aliambiwa na mke wake waende kliniki pamoja, Baba akasema mambo hayo ni yawanawake hivo yeye hawezi kwenda,

Mke wake alivyoenda kuanza kliniki hudhurio la kwanza, wahudumu wa afya wakawa wamewapa kipaombele wajawazito ambao wamekuja na waume zao,

na Lengo ilikuwa ni kutoa hamasa kwa wakina baba kuhudhuria kliniki.

Na siku hyo wagonjwa walikuwa wengi sana ikiwemo wajawazito walikuwa wamejaa hospitalini, hali ambayo ikapelekea mke wake kuchelewa kurudi nyumbani,

Baba akauliza ” kulikoni leo mbona kliniki ya leo mimi sielewi?”

Mama akajibu ” Wajawazito wote ambao wamekuja na waume zao wamepewa kipaumbele hivo wamewahi kurudi nyumbani,sisi ambao tupo peke yetu tumekuwa wamwisho kupata huduma”

Baba akasikitika sana akasema” Kliniki ijayo tutaenda wote nione nini kinaendelea hapo kwenye hayo mambo yenu ya kike”

Basi hudhurio la pili la kliniki likafika, Na mapema Baba akasisitiza kwamba siku hyo lazima amsindikize mke wake hospitalini,

Basi wakaamka mapema na kujiandaa wote kwenda kliniki, baada ya kufika hospitalini wakawa watu wa kwanza kabsa kuanza kuhudumiwa.

Mbali na hyo” Baba mwenyewe akaanza kupewa elimu ya afya na umuhimu wa yeye kwenda kliniki na mke wake”

siku hyo baba alipata package ya kutosha na kuwa mwalimu wa mke wake.

Tangu siku hyo, baba akawa ameelewa umuhimu wa kuhudhuria kliniki yeye na mke wake, nakujua hayo sio mambo ya kike au wanawake pekee yao.

Baada ya kupewa elimu yakutosha na kupewa dawa za kuongeza damu maarufu kama FEFOL, wakarudi nyumbani, kufika nyumbani baba akakagua dawa walizopewa hospitalini ambazo waliambiwa kwamba zina umuhimu mkubwa ikiwemo; kuongeza damu, kupunguza tatizo la kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa pamoja na mgongo wazi.

Kuziangalia zile dawa akagundua zilifanana na zile za kipindi kile ambazo mke wake alipewa kwenye mimba ya kwanza, na Yeye hakumuelewa mke wake na kumuambia aache kuzitumia hali ambayo ilichangia kwa kiasi kikubwa kuzaa mtoto mwenye shida ya mgongo wazi yaani spinal bifida.

Wakati yeye alimkataza mke wake kutumia zile dawa,wala dawa zingine zozote, na hata kliniki alitaka asiende.

STORIES HII Inatufundisha kwamba,Unaweza kuwa mbishi kwa kukosa elimu, lakini ukipata elimu itakuwa msaada kwako na kwawengine.

Kilinichomfanya baba huyu kugoma kwa kila kitu,ni kwasababu alikosa elimu ya kutosha kuhusu umuhimu huu wa kliniki kwao wawili, hali ambao ulimfanya atawaliwe na Imani POTOFU kwa kila ktu.

Lakini baada ya kupata elimu ya kutosha baba huyu alikuwa mwalimu na msaada kwa Mke wake wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua.

KUNA FAIDA NYINGI SANA ZA KUDHURIA KLINIKI KWA WOTE WAWILI IKIWEMO;

– Kupata elimu ya kutosha ya afya ya uzazi,

• matunzo ya mimba,

• maandalizi ya kujifungua,

• Kujua dalili za hatari wakati wa ujauzito, nakusaidiana kukumbushana

– Upimaji wa magonjwa mbali mbali kama vile Ukimwi n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.