Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

DHANA POTOFU KUHUSU UCHANGIAJI DAMU

KUCHANGIA DAMU HAKUNA MADHARA(soma hapa)

Watu wengi au jamii nyingi zimekuwa zikishikilia dhana potofu kwamba uchangiaji damu una madhara makubwa mwilini,

na mtu akichangia damu itamlazimu kufanya hivyo kila mara.

DHANA POTOFU KUHUSU UCHANGIAJI DAMU

-Mtu akichangia damu itasababisha damu kuongezeka kila mara na kumlazimu kutoa damu kila wakati kwenye maisha yake yote.

Dhana hii ni potofu na imekuwa ikiwapa shida sana watu wanaohamasisha mpango wa uchangiaji Damu Salama.

FAHAMU HILI; Kulingana na maumbile ya Mwanaume yalivyo, Mwanaume ana uwezo wa kuchangia damu kila baada ya Miezi 3 Bila kupata shida yoyote,

Na mwanamke ana uwezo wa kuchangia damu kila baada ya Miezi 4 bila shida yoyote.

Kama mtu ana shida ya damu kuongezeka akutane na wataalam wa maswala ya Damu kuangalia kwanini chembe chembe zake za damu zinajizalisha kupita kiasi na kupata Tiba sahihi,

Lakini atambue hakuna uhusiano wa kuchangia damu na damu kuongezeka kwa wingi.

Vitu ambavyo huzingatiwa wakati wa uchangiaji damu ni pamoja na Kupima Uzito wa mwili, Presha N.K.

EPUKA IMANI POTOFU CHANGIA DAMU OKOA MAISHA.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.