Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

KUCHAMBA KWA MAJI MACHAFU MADHARA YAKE

KUCHAMBA KWA MAJI MACHAFU MADHARA YAKE,

Kwa ujumla mazingira ya chooni(toilet) hutakiwa kuwa masafi sana ikiwemo vyombo ambavyo huweza kutumika kwenye eneo hili,

Asilimia kubwa sana ya Vimelea vya magonjwa unaweza kuvipata chooni kama usipokuwa muangalifu.

Na kwa wale ambao wanatumia vyoo ambavyo lazima uweke chombo cha maji kama vile ndoo,makopo n.k

Unatakiwa kuhakikisha vyombo hivo ikiwemo ndoo pamoja na makopo vinakuwa visafi muda wote,

epuka tabia ya kuongeza maji juu ya maji mengine ambayo yamekaa kwa muda mrefu kwenye ndoo, Hapa unazidi kuweka mazingira mazuri kwa vimelea wa magonjwa kama vile bacteria kuendelea kuzaliana.

Ukiwa chooni Unaweza kupata vimelea vya magonjwa kama vile bacteria,Uwepo wa Fangasi,Minyoo n.k

KUCHAMBA KWA MAJI MACHAFU MADHARA YAKE,

– Unajiweka kwenye hatari ya kupata maambukizi kama vile UTI,

na hii hutokea kwa kiasi kikubwa kwa Wanawake kutokana na maumbile yao yalivyo.

Mbali na kwamba,tabia ya kuchamba kutoka nyuma kwenda mbele unaweza kupata vimelea vya magonjwa kama vile bacteria kutoka kwenye njia ya haja kubwa kwenda ukeni,

Hata kutumia maji machafu pia unaweza kupelekea vimelea hawa kuingia Ukeni,

– Harufu mbaya kutoka sehemu za Siri, baada ya kutumia maji machafu ukiwa toilet huweza kusababisha harufu mbaya kutoka sehemu zako za Siri hasa pale ukitoa jasho.

– Maambukizi ya Fangasi, Pia unaweza kupata Fangasi sehemu za siri kama unatumia maji machafu mara kwa mara

– Hali ya muwasho usioisha hasa kwenye eneo la Msamba( kati ya haja kubwa na haja ndogo) ambalo kwa kitaalam hujulikana kama perineum N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.