Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO PAMOJA NA MIKOA INAYOONGOZA

UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO PAMOJA NA MIKOA INAYOONGOZA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka watoto kote nchini kufichua viashiria vya vitendo vya kikatili dhidi yao vinavyotokea hasa katika maeneo ya shule na nyumbani.

#KuelekeaSikuyaMtotowaAfrika “Watoto kote nchini fichueni viashiria vya vitendo vya kikatili dhidi yao vinavyotokea hasa katika maeneo ya shule na nyumbani” Waziri Dkt Gwajima

“Niwaombe watoto kutokuogopa na badala yake waonapona vitendo vya ukatili au viashiria watoe taarifa kwa watu wanao waamini ikiwepo dawati la jinsia linalopatikana kwenye vituo vya Polisi”

”Wanangu, Baba akikukatli mwambie Mama na kama ni Mama basi mwambie Baba, au kama unaona huwezi kumwambia Baba au Mama basi mwambie mtu unayemwamini”

“Matukio ya ukatili kwa watoto katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2021, jumla ya matukio yaliyoripotiwa ndani ya Jeshi la Polisi ni 11,499 ikilinganishwa na matukio 15,870 katika kipindi kama hicho mwaka 2020″

“Mikoa ya kipolisi inayoongoza kwa ukatili ni Arusha (808), Tanga (691), Shinyanga (505), Mwanza (500) na Ilala (489) na makosa yaliyoongoza kwa idadi kubwa ni ubakaji (5,899), mimba kwa wanafunzi (1,677) na ulawiti (1,114)” Waziri Dkt. Gwajima.

Piga simu no: 116 Popote pale ulipo nchini, Ripot ukatili wowote Kwa watoto

KWA PAMOJA TUNAWEZA KUDHIBITI VITENDO HIVI.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.