Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

ULAWITI,UBAKAJI,KUPATA MIMBA KWA WANAFUNZI(ukatili wa Kijinsia)

ULAWITI,UBAKAJI,KUPATA MIMBA KWA WANAFUNZI(ukatili wa Kijinsia)

Haya ni miongoni mwa matukio ya ukatili kwa watoto ambayo yanatokea kwa wingi,

Na Kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika Waziri Dkt. Gwajima amesema haya “Mikoa ya kipolisi inayoongoza kwa ukatili ni Arusha (808), Tanga (691), Shinyanga (505), Mwanza (500) na Ilala (489)

na makosa yaliyoongoza kwa idadi kubwa ni ubakaji (5,899), mimba kwa wanafunzi (1,677) na ulawiti (1,114)”

Ukatili huu ni wakupiga vita sana, na kila mmoja analojukumu la kuhakikisha vitendo hivi havitokei,

maana leo kwa jirani kesho ni kwako, je utakuwa kwenye hali gani endapo ukatili huu umetokea ndani ya Familia yako?

Madhara ya Ukatili huu ni makubwa kwa watoto wetu na Jamii kwa ujumla,

• ikiwemo kuwaweka watoto kwenye hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na magonjwa mengine ya Zinaa

• Kupoteza kabsa tumaini la kuishi

• Kutokujiamini tena mbele za watu

• Kuwa na hofu kubwa, wasi wasi pamoja na msongo wa mawazo

• Kufeli masomo yao na kupoteza kabsa Dira ya maisha

• Watoto kupata mimba kwenye umri mdogo sana

• Kupoteza maisha N.k

Tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha ukatili huu unaisha kabsa.

Piga simu no: 116 Popote pale ulipo nchini, Ripoti ukatili wowote Kwa watoto

KWA PAMOJA TUNAWEZA..!!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.