Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANZO CHA MAUMIVU YA MGONGO NA TIBA YAKE

CHANZO CHA MAUMIVU YA MGONGO NA TIBA YAKE

Watu wengi hupata tatizo la maumivu ya mgongo kwa vipindi tofauti kwenye maisha yao, je unajua sababu ambazo huweza kuchangia wewe kuwa na maumivu ya mgongo? soma hapa.

Katika Makala hii tumechambua Zaidi kuhusu Sababu au chanzo cha maumivu ya mgongo, Pamoja na Matibabu yake;

BAADHI YA SABABU ZINAZOCHANGIA MAUMIVU YA MGONGO NI PAMOJA NA;

– Kupata ajali au kuumia(Injury), Kuumia huku huweza kuhusisha misuli pamoja na Ligaments kuvutwa zaidi, kupata shida ya muscle spasms au damaged disks kwenye pingili za uti wa mgongo,

vyote hivi huweza kusababisha tatizo la maumivu ya mgongo kwa mhusika.

– Kufanya kazi mbali mbali,kunyanyua vitu isivyosahihi, kunyanyua vitu vizito sana, Kujivuta zaidi,kujikunja zaidi n.k

– Sababu zingine zinazoweza kupelekea tatizo la maumivu ya mgongo ni Pamoja na;

  1. kusimama kwa muda mrefu sana,
  2. kukaa kwa muda mrefu sana,
  3. kuendesha gari umbali mrefu sana bila kupumzika,
  4. Kulala vibaya,
  5. kulala kwenye godoro ambalo halisupport pingili za mgongo kunyooka vizuri(keep spine straight) n.k

– Tatizo la Osteoarthritis,Osteoporosis, au matatizo ambayo huathiri Nerves kama vile shingles Infections n.k

– Sababu zingine ni pamoja na;

• Ugonjwa wa kansa yaani Spine cancer

• Maambukizi kama vile; Pelvic Inflammatory disease(PID),

• maambukizi kwenye kibofu cha Mkojo pamoja na maambukizi kwenye figo (UTI),

• Tatizo la mawe kwenye figo(Kidney stones) n.k

SABABU AMBAZO HUWEZA KUONGEZA UWEZEKANO WA WEWE KUPATA TATIZO LA MAUMIVU YA MGONGO(Risk factors)

– Kazi mbali mbali unazofanya zinazohusisha kusimama muda mrefu,kukaa sana, kujikunja sana, kunyanyua vitu vizito n.k

– Kuwa mjamzito

– Kufanya mazoezi vibaya

– Kuwa na umri mkubwa(uzee)

– Kuwa na shida ya uzito mkubwa sana(Overweight/Obesity)

– Uvutaji wa Sigara,

– Matatizo kama arthritis na cancer

FAQs: Maswali ambayo huulizwa Mara kwa mara

Je, Mama mjamzito anaweza kupata tatizo la maumivu ya mgongo?

Ndyo, Moja ya kundi la watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata tatizo la maumivu ya mgongo ni pamoja na wanawake wajawazito.

Hitimisho:

Maumivu ya mgongo ni tatizo ambalo husumbua watu wengi zaidi,

Na moja ya kundi ambalo lipo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la maumivu ya mgongo ni pamoja na;

  • Wazee
  • Wanaofanya kazi za kusimama kwa muda mrefu zaidi
  • Wanaofanya kazi za kukaa kwa muda mrefu zaidi,mfano madereva wa magari ya masafa marefu n.k
  • Wenye Uzito mkubwa
  • Wanaonyanyua Vitu vizito Zaidi n.k

Kwa asilimia kubwa Sababu za maumivu ya mgongo huweza kuzuilika,mfano; kama unafanya kazi za kukaa muda mrefu hakikisha unapata muda wa  kufanya mazoezi, kama una Uzito mkubwa hakikisha unapungua,epuka uvutaji wa Sigara, epuka Kuvaa viatu vyenye visigno virefu zaidi n.k.

Lakini kama bado tatizo linaendelea licha ya Kuzingatia hatua hizi, Hakikisha unapata msaada wa matibabu kutoka kwa Wataalam wa afya. Au

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.