Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Muwasho kwenye njia ya mkojo unaoambatana na mkojo wenye harufu kali

Muwasho kwenye njia ya mkojo unaoambatana na mkojo wenye harufu kali

Ukipatwa na maambukizi ya vimelea vya magonjwa(infections) kama Bacteria n.k kwenye eneo lolote ndani ya Njia ya Mkojo(Urinary tract),

Huweza kusababisha rangi ya mkojo kubadilika pamoja na Mkojo kuwa na harufu kali, harufu hii sio sawa na ile ambayo unaweza kuisikia baada ya kunywa baadhi ya dawa.

CHANZO CHA MUWASHO KWENYE NJIA YA MKOJO UNAOAMBATANA NA MKOJO WENYE HARUFU KALI

Kama nilivyokwisha kueleza hapo mwanzo, uwepo wa hali kama hizi;Muwasho unaombatana na Mkojo kutoa harufu kali ni dalili za maambukizi kwenye eneo la Njia ya Mkojo yaani Urinary tract,

je maambukizi haya yanatokana na nini? Unaweza kupata maambukizi mbali mbali ikiwemo;

– Maambukizi kwenye njia ya mkojo au Tatizo la UTI, ambayo huweza kusababisha muwasho kwenye njia ya mkojo, mkojo kuwa na harufu kali, Uume kuwa wamoto sana n.k

– Magonjwa mbali mbali ya zinaa(Sexual transmitted diseases-STD’s) kama vile; Kisonono(gonorrhea), Chlamydia, trichomoniasis n.k

– Wakati mwingine tatizo la Fangasi huweza kupelekea miwasho mikali kwa nje na hata mpaka kwenye njia ya Mkojo.

– Tatizo la Urethritis, ambapo huhusisha kuvimba kwa Urethra chanzo kikiwa maambukizi ya magonjwa kama UTI, tatizo hili pia huweza kusababisha;

• Kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa

• kupata miwasho karibu kabsa na tundu la mkojo

• Uwepo wa damu kwenye mkojo au shahawa n.k

Chanzo kikubwa cha tatizo la urethritis ni maambukizi ya Bacteria au Virusi, ila Bacteria ndyo huchangia kwa kiwango kikubwa zaidi,

Kutokana na “Centers for Disease Control and Prevention (CDC)” bacteria ambao husababisha kwa kiasi kikubwa tatizo la urethritis ni pamoja na:

✓ Neisseria gonorrhoeae

✓ Chlamydia trachomatis

✓ Mycoplasma genitalium

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.