Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Umekuwa ukisikia habari ya kufanya Mazoezi ya Mwili Mara kwa mara

Umekuwa ukisikia habari ya kufanya Mazoezi ya Mwili Mara kwa mara,

Na pengine hujui kwanini watu wanasisitizwa kufanya mazoezi, hata wakina mama wajawawazito na ambao wamejifungua hasa kwa Upasuaji wote wanashauriwa kufanya mazoezi,

Mazoezi ni afya, mazoezi ni kinga,mazoezi ni Tiba

• Kama ulikuwa hujui mazoezi husaidia sana kuboresha na kuimarisha kinga yako ya mwili,

na kukufanya usiwe mtu wa kuumwa umwa mara kwa mara

• Mazoezi yanaweza kukukinga na magonjwa mbali mbali ikiwemo Ugonjwa wa Presha au shinikizo la Damu,kisukari,magonjwa ya moyo n.k

• Mazoezi husaidia sana kuboresha  mzunguko wa damu, na kukusaidia kupona haraka vidonda, mfano kwa mama aliyejifungua kwa njia ya upasuaji

• Mazoezi husaidia kuondoa stress au msongo wa mawazo

• Mtu ambaye hufanya mazoezi hata uwezo wake wa kufikiri huwa mkubwa

• Mazoezi husaidia kupata usingizi mzuri

• Mazoezi husaidia kupunguza Uzito N.k

Na faida zingine Lukuki ambazo zijazitaja hapa,

Fanya mazoezi kila siku, angalau kwa dakika 30 au Nusu saa kwa ajili ya kuboresha afya yako

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.