Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Jamii Izingatie Mambo Haya ili kuepuka Kupata Ugonjwa wa Kisukari

Jamii Izingatie Mambo Haya ili kuepuka Kupata Ugonjwa wa Kisukari,

Fahamu Baadhi ya mambo kuhusu Ugonjwa huu wa Kisukari kupitia kwenye makala hii,pamoja na vitu vya kuzingatia

Ugonjwa wa kisukari huweza kutokea kwa mtu yoyote,japo kuna makundi ya watu ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa kisukari na makundi hayo ni kama vile;

• Wenye historia ya watu kuumwa kisukari katika familia zao

• Wenye tatizo la uzito kupita kiasi au Overweight.

• Wenye shida ya Presha au shinikizo la damu

• Wenye tatizo la kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu au Cholesterol mwilini

• Wanawake wenye tatizo la Polycystic ovarian syndrome (PCOS)

• Wanawake wenye historia ya kupatwa na tatizo la Kisukari kipindi cha ujauzito yaani gestational diabetes.

HIZI HAPA NI BAADHI YA SABABU AMBAZO HUONGEZA KIWANGO CHA SUKARI KWENYE DAMU KWA WATU AMBAO TAYARI WANAUGONJWA WA KISUKARI

– Kutokutumia dose sahihi ya Insulin au dawa sahihi za kumeza kwa ajili ya ugonjwa wa kisukari

– Mwili wako kuacha kutumia Insulin asilia iliyopo mwilini hasa kwa type 2 diabetes

– Kiwango cha carbohydrates unachokula au kunywa hakiendani na kiwango cha Insulin ambayo mwili wako hutengeneza au Kiwango cha Insulin inachopewa kupitia dawa(sindano)

– Mgonjwa kuanza kuwa na tatizo la Msongo wa mawazo,hofu au wasiwasi kutokana na ugonjwa uliompata au kitu kingine chochote,huweza kuathiri kiwango cha sukari kwenye damu ndani ya mwili wako

– Matatizo kwenye Endocrine huweza kusababisha tatizo la Insulin kushindwa kufanya kazi

– Magonjwa mbali mbali yanayohusisha Kongosho(Pancrease) kama vile; cystic fibrosis au tatizo la kansa ya kongosho

– Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile; dawa jamii ya diuretics,steroids n.k

BAADHI YA DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI(SUKARI KUZIDI KWENYE DAMU)

1. Mtu kuwa na kiu ya maji sana kupita kawaida au kupata njaa sana mara kwa mara

2. Mtu kutokuona vizuri pamoja na kupatwa na tatizo la kuona marue rue

3. Mtu kuanza kukojoa mara kwa mara kuliko kawaida

4. Mtu kupatwa na tatizo la maumivu makali ya kichwa mara kwa mara shida ambayo haikuwepo hapo mwanzo

5. Mwili kuchoka kuliko kawaida pamoja na uzito wa mwili kupungua kwa kasi sana

6. Wengine hupatwa na maambukizi ya magonjwa kwa urahisi sana kama sehemu za siri(ukeni) pamoja na kwenye ngozi

7. Kuwa na tatizo la vidonda kuchelewa kupona kuliko kawaida n.k

JINSI YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA KISUKARI

Hizi hapa ni baadhi ya njia mbali mbali ambazo zitakusaidia wewe kujikinga na ugonjwa huu wa kisukari

✓ Fanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 au Nusu saa kwa siku, tafiti zinaonyesha kwamba mazoezi ni njia nzuri ya kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu pamoja na kuzuia magonjwa mbali mbali kama vile; ugonjwa wa Kisukari,presha,magonjwa ya moyo n.k

✓ Kula mlo kamili,mlo wenye virutubisho vyote kwa kiwango sahihi kinachohitajika mwilini, epuka matumizi ya sukari kupita kiasi au kula vyakula vya wanga mwingi kuliko vyakula vingine

✓ Hakikisha unakuwa na uzito sahihi na kuepuka matatizo kama vile; kuwa na uzito mkubwa(overweight) au kuwa mnene kupita kawaida

✓ Epuka tabia hatari ya uvutaji wa Sigara

✓ Epuka kabsa matumizi ya pombe au Dhibiti sana matumizi ya Pombe, Tafiti zinaonyesha kwamba Pombe inaweza kuongeza kiwango cha Sukari kwenye damu ndani ya mwili wako

N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.