Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Kijiti cha Uzazi wa Mpango kinaanza kufanya kazi baada ya Muda gani?

Kijiti cha Uzazi wa Mpango kinaanza kufanya kazi baada ya Muda gani?

Ifahamike kwamba kuna kijiti kinachozuia Mimba kwa Muda wa Miaka 3, na vile vya Miaka 5,

Hivo kama umepanga kutumia Njia hii kwa ajili ya kupanga Uzazi unatakiwa kufahamu hilo,

Sasa basi, Baada ya kuweka Kijiti cha Uzazi wa Mpango,Je kinaanza kufanya kazi baada ya Muda gani toka uweke?

Kijiti hiki kitaanza kufanya kazi haraka zaidi na kuzuia mimba bila wasi wasi wowote kama kimewekwa ndani ya siku 5 za kwanza toka siku ya kwanza ya kuona hedhi yako,

Ingawa unaweza kuweka muda wowote unaotaka wewe mara tu baada ya kupimwa na kuonekana huna Mimba.

Lakini kwa Case kama hii ya kuweka kijiti nje ya zile siku 5 toka siku ya kwanza ya kuona hedhi, Utendaji kazi wa kijiti utakuwa vizuri zaidi baada ya siku 7 toka uweke,

Hivo basi unashauriwa kuendelea kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kutumia kinga kama Condom ndani ya siku hizi 7 baada ya kuweka kijiti chako.

Hapo utakuwa na uhakika zaidi na kujikinga na Mimba zisizotarajiwa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.