Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Madhara ya Kuzaa Mapema Kwa Mwanamke na Mtoto

Madhara ya Kuzaa Mapema Kwa Mwanamke na Mtoto

Kuanza kushiriki tendo la ndoa kabla ya kufikia umri wa miaka 18, na wengine kuanza kubeba Mimba na Kuzaa wakiwa na umri mdogo sana,vyote hivi vina madhara kiafya,kiuchumi na kijamii pia.

– Tafiti zinaonyesha Wanawake ambao huanza kufanya mapenzi mapema sana au kabla ya kufikia Umri wa Miaka 18,

Wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi(Cervical Cancer)

(1) Madhara kwa Mwanamke ni pamoja na;

• Kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa mbali mbali, ikiwemo Sararani ya Kizazi na magonjwa mengine kama ya Zinaa n.k

• Kuwa kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la FISTULA,

Tatizo hili huwasumbua Wanawake wengi, hasa wale ambao hujifungua kwenye umri mdogo sana

• Kuchanika Sana wakati wa kujifungua pamoja na kuvuja damu nyingi

• Kuwa kwenye hatari zaidi ya kujifungua kwa njia ya UPASUAJI

• Kupoteza Maisha wakati wa Kujifungua n.k

(2). Madhara kwa Mtoto ni pamoja na;

• Mtoto kuzaliwa kabla ya Wakati(premature birth)

• Mtoto kuzaliwa na tatizo la uzito mdogo sana(low birth weight)

• Mtoto kupoteza maisha wakati wa kuzaliwa,

Mara nyingi hii huweza kutokea pale ambapo Njia ya Mama anayejifungua ni ndogo sana wala viungo vyake vya uzazi havijakomaa vizuri,

hali ambayo hupelekea mtoto kupata shida sana kutoka, wakati wa kuzaliwa,

na endapo hakuna msaada wa haraka au mama huyu akawa anajaribu kuzaa kawaida akiwa nyumbani, huweza kumpoteza mtoto wake,na yeye mwenyewe pia.

EPUKA KUBEBA MIMBA NA KUZAA KWENYE UMRI MDOGO, #STOP #TEENAGEPREGNANCY

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.