Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Madhara ya Uvutaji wa Sigara Kwa Wanawake na Wanaume(Vifo kutokana na Nimonia)

Madhara ya Uvutaji wa Sigara Kwa Wanawake na Wanaume(Vifo kutokana na Nimonia)

Fahamu Kuacha kuvuta sigara kwa kiasi kikubwa kunapunguza hatari ya vifo kutokana na nimonia;

Je ni madhara yapi unaweza kuyapata kwa Kuvuta Sigara? Haya hapa ni baadhi ya Madhara kwa Wanaume na Wanawake.

MADHARA YA MWANAMKE KUVUTA SIGARA

Madhara ya uvutaji wa sigara ni kwa kila mtu anayevuta bila kujalisha umri au jinsia, japo kuna madhara mengine huwa maalum kwa jinsia flani,

katika makala ya leo tunazungumzia madhara ya Uvutaji wa sigara Kwa kuangalia jinsia(Wanawake na Wanaume).

MADHARA YA MWANAMKE KUVUTA SIGARA NI PAMOJA NA;

1. Uvutaji wa sigara huweza kumuweka mwanamke katika hatari ya kupata shida ya mimba kutunga nje ya kizazi yaani kwa kitaalam tunaita Ectopic pregnancy

2. Uvutaji wa sigara kwa mwanamke huweza kumsababishia kuwa katika hatari ya kupatwa na shida ya kansa mbali mbali ikiwemo kansa ya Mapafu n.k

3. Mwanamke kuzaa watoto wenye tatizo la uzito mdogo sana kuliko kawaida(uzito wa kawaida Kgs 2.5 mpaka 3.5)

4. Mwanamke kuwa katika hatari ya kupatwa na tatizo la mvuruguko wa vichocheo vya mwili yaani kwa kitaalam tunaita hormone imbalance

5. Mwanamke kupatwa na shida ya kutokubeba mimba au kupata tatizo la kushika ujauzito na kutoka wenyewe

6. Kuzaa watoto wenye matatizo katika mfumo mzima wa upumuaji

7. Mwanamke kuzaa watoto wenye shida ya figo

8. Mwanamke kuzaa watoto na kufariki muda mfupi baada ya kuzaliwa

9. Uvutaji wa sigara huweza kusababisha matatizo ya mapafu ikiwa ni pamoja na Kansa ya mapafu

10. Kupatwa na shida ya koo ikiwa ni pamoja na kupatwa na kansa ya Koo

11. Kupunguza Hamu ya Tendo la Ndoa

N.K

ONYO; uvutaji wa Sigara ni hatari kwa afya yako na afya ya mtoto wako

MADHARA YA MWANAUME KUVUTA SIGARA;

-Uvutaji Wa Sigara Hupunguza Nguvu Za Kiume

– Pamoja na Kupunguza hamu ya tendo la ndoa

Moja ya madhara makubwa ya uvutaji wa sigara ni pamoja na kupunguza hamu ya tendo la ndoa kwa wote(wanaume na wanawake).

– Uvutaji wa sigara kwa wanaume hupunguza hamu ya tendo la ndoa kwa kupunguza kiwango cha uzalishaji wa vichocheo aina ya testerone mwilini, hivo kumfanya mwanaume asiwe na hamu ya tendo la ndoa.

– Pia madhara mengine ya uvutaji wa sigara kwa Wanaume ni kupunguza nguvu za kiume. Hii ni kutokana na kwamba uvutaji wa sigara huathiri mzunguko mzima wa damu katika uume,hivo kuufanya uume ushindwe kusimama vizuri na kufanya kazi kama kawaida.

– Pia sigara huathiri utengenezaji wa mbegu za kiume pamoja na uzito wa mbegu,hivo kumuweka mwanaume mvutaji kwenye hatari ya kushindwa kumpa mwanamke mimba.

– Uvutaji wa sigara unahusishwa na kuharibu shape ya mbegu za kiume,hivo kusababisha mbegu nyingi kufa.

– Pia uvutaji wa sigara huhusika na kuharibu vishipa vidogo ambavyo mbegu hutengenezwa na kupita hapo,hivo kuendelea kusababisha tatizo la mbegu chache kupita.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.