Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Moja ya vitu ambavyo huweza kupunguza Maumivu ya Mgongo ni pamoja na kulala Upande

Moja ya vitu ambavyo huweza kupunguza Maumivu ya Mgongo(Back Pain) ni pamoja na kulala Upande,

Hii inasaidia kupunguza maumivu ya mgongo, na wengine huweka mto katikati ya miguu,hii ni bora zaidi pia.

Je vitu gani hupelekea Shida ya Maumivu ya Mgongo?

CHANZO CHA MAUMIVU YA MGONGO NA TIBA YAKE

Watu wengi hupata tatizo la maumivu ya mgongo kwa vipindi tofauti kwenye maisha yao, je unajua sababu ambazo huweza kuchangia wewe kuwa na maumivu ya mgongo? soma hapa

BAADHI YA SABABU ZINAZOCHANGIA MAUMIVU YA MGONGO NI PAMOJA NA;

– Kupata ajali au kuumia(Injury), Kuumia huku huweza kuhusisha misuli pamoja na Ligaments kuvutwa zaidi, kupata shida ya muscle spasms au damaged disks kwenye pingili za uti wa mgongo

– Kufanya kazi mbali mbali,kunyanyua vitu isivyosahihi, kunyanyua vitu vizito sana, Kujivuta zaidi,kujikunja zaidi,

– kusimama kwa muda mrefu sana, kukaa kwa muda mrefu sana, kuendesha gari umbali mrefu sana bila kupumzika, Kulala vibaya, kulala kwenye godoro ambalo halisupport pingili za mgongo kunyooka vizuri(keep spine straight) n.k

– Tatizo la Osteoarthritis,Osteoporosis, au matatizo ambayo huathiri Nerves kama vile shingles Infections n.k

– Sababu zingine ni pamoja na;

• Ugonjwa wa kansa yaani Spine cancer

• Maambukizi kama vile; Pelvic Inflammatory disease(PID), maambukizi kwenye kibofu cha Mkojo pamoja na maambukizi kwenye figo (UTI), Tatizo la mawe kwenye figo(Kidney stones) n.k

SABABU AMBAZO HUWEZA KUONGEZA UWEZEKANO WA WEWE KUUMWA MGONGO(Risk factors)

– Kazi mbali mbali unazofanya zinazohusisha kusimama muda mrefu,kukaa sana, kujikunja sana, kunyanyua vitu vizito n.k

– Kuwa mjamzito

– Kufanya mazoezi vibaya

– Kuwa na umri mkubwa(uzee)

– Kuwa na shida ya uzito mkubwa sana(Overweight/Obesity)

– Uvutaji wa Sigara,

– Matatizo kama arthritis na cancer

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.