Tatizo la Kunuka Kikwapa chanzo chake
Tatizo la Kunuka Kikwapa chanzo chake
Kuna takribani tezi za jasho yaani Sweat glands Million 2 mpaka 4 kwenye mwili wa binadamu,
Na kwa asilimia kubwa ni tezi aina ya Eccrine sweat glands pamoja na Apocrine sweat glands, Na tezi hizi mbili za jasho kwa asilimia kubwa zipo kwapani(armpits),
Wakati mtu akifanya mazoezi au mwili kupata joto sana,Tezi za jasho hutoa jasho kwa lengo la kupoozesha mwili wako,
Lakini pia msongo wa mawazo au Stress,woga,hofu,wasiwasi,hasira au hisia kali huweza kusababisha tezi hizi kutoa jasho
– Tezi za jasho yaani Sweat glands huwa active zaidi wakati binadamu akifikia umri au kipindi cha Balehe maarufu kama puberty,
Na hapa ndipo wadada kwa wakaka huanza kutoa jasho lenye harufu,
– Baadhi yao hupatwa na shida nyingine ya kutoa jasho kupita kiasi,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Hyperhidrosis,
Tatizo hili huhusisha mwili kutoa jasho jingi sana kuliko kawaida, ila halina harufu mbaya, na hutokea kwa wastani wa asilimia 3% ya watu
– Endapo unatokwa na jasho lenye harufu mbaya au kali,licha yakutumia deodorant au kufanya usafi wa mwili,hilo ni tatizo
CHANZO CHA KUTOA JASHO LENYE HARUFU MBAYA NI PAMOJA NA;
• Kutokufanya usafi wa mwili vizuri au kutokuoga yaani poor hygiene
• Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile;
– Uwepo wa maambukizi ya Bacteria
– Tatizo la Fangasi wa kwenye ngozi,kwapani,kwenye damu n.k
MATIBABU YA TATIZO LA KUTOA JASHO LENYE HARUFU MBAYA
Kwanza kabsa kama una tatizo hili unashauriwa kuhakikisha unakuwa msafi muda wote,na kutumia vitu kama deodorant zenye harufu nzuri,
Pata tiba ya magonjwa kama vile Fangasi,bacteria n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.